Tetesi:Mgomo unanukia udsm.

hv kuna tofauti kiakili kati ya mpiga msuli na perry??

TAperry huwa ana akili za usiku tu,hajawahi kuwa na akili za mchana! tofauti na Mpiga msuli(masterpweele) yeye mara chache anakuwa na akili za mchana.
 
Nyie endeleeni kuleta mbwembwe hapo za hiyo migomo na mobilization zisizo na maana,kuna mwana nakumbuka nilipokua nasoma hapo UDSM,alikua mtata sana na organiser wa migomo,alikua anajiita ALSHABABI ilikua mwaka 2012 aliusumbua sana uongozi wa chuo maana wenzie wote walikua wamesimamishwa chuo yeye ndio akawa amebakia na akawa anaongoza iyo migomo,unaambiwa usalama wa taifa walikua wanamsaka sana,ila mara ya mwisho nakumbuka alikuja kuchukuliwa saa nane za usiku pale mabibo hosteli na watu wasiojulikana hadi leo sijui aliishia wapi............so kuweni makini.
 
Reactions: SJA

Jamaa alitamba sana... dada mmoja mchaga nae akaunga mkono harakati akajiita ALSHABIBI sijui kapotelea wapi....
 

Duh kumbe vyuoni kuna mambo.
 
ALSHABAB ndo alikua mtu wa mwisho kumobilize mgomo pale chuoni tokea uongozi umshuhulikie hakuna kiumbe mwingine aliejitokeza kumobilize watu....buriani revo square!
 

Ni mmoja wa muanga wa mgomo wa 2010/11/2012 na kwasasa nipo kwenye moja ya vyuo vikuu napiga shule....niliwahi kuchukuliwa na usalama kwa maoijiano na kwa ajili ya kufanya mgomo usitokee ila badae walituachia tukiwa watu kumi kwani tulikuwa tukiandaa mgomo pale mabibo block G na kwakweli tulifanikiwa sana kwani bumu liliweza kupanda na vijana waliokosa mkopo waliweza kupata...uoga haujawahi kushinda na tatizo kubwa la vyuo vyetu watu wanajidai wasome wamalize waondoke...toeni uoga vijana wa udsm na vyuo vingine piganieni haki yenu´....sitawasahau vijana wafuatao waliowezesha harakati zile Richard marwa,makwaiya,ndunguru florian,ndunguru francis,emekha lusako,alshabib,alshabab n.k. Na wengine waliojitolea tuzo yetu ni kubwa.....na kwa ufupi alshabab yupo hai na anaendelea vizuri na hao wengine wote wapo hai wanapiga shule...
 
Mkigoma mnamgomea nani?kuna mtu anajali kuathirika kwenu kielimu?Kuna watu walisoma hadi leo ni madaktari na maprof. lakini hao ndio wanafanya mambo ya kikanjanja hadi nyie leo mnacheleweshewa "boom"kama mnavyoita wenyewe!Nawashauri mtafute njia nzuri ya kudai haki zenu kwani ni wazi Tanzania watu wengi wakisoma wanakuwa Sadists!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Sisi hatunaga tambo huo ni uongo mtupu haya hayakuhusu yaache yalivyo, acha kuleta ushabiki kwenye mambo usiyoyajua.
 
Kitaeleweka tu,leo nimeshuhudia waraka wa raisi KISANKO nadhani tukiungana flan hv ishu itasovika..ngoja nirudi bibo
 

Ni kweli unachosema mkuu....watu wanashindwa kuelewa kua cku zote ktk kupigania haki lazima kuwe na gharama ili hiyo haki ipatikane....tunasahau hta kua hta yesu ilibdi ateseke na afe ili atambuliwe kua ni mfalme wa wayahudi...hizi kauli za kebehi hazifai kabisa kwasababu hali waliyonayo wanafunzi wa vyuo vyte nchini ni kwasababu ya migomo flani iliyotokea kipindi cha nyuma na pesa ya matumizi kuongezwa
 

Uoga wako ndio umasikini wako....binadamu ni kiumbe kinachoweza kuishi kwa matumaini kwa muda mrefu sana ila aonapo mbele giza basi huwa mkatili....katika maisha ukiwa muoga kila cku hutakaa kuthubutu kitu
 

Kwa ushauri wako wewe ni njia gani zingine zinafaa??
 
dogo msijali pigeni mzigo hadoi kieleweke.eboo bila mgomo hao jamaa tushawazoea tangu 2008
 
Wamesharudishwa mfano udom aliyewahi kuwa raisi wa wanafunzi na serikali yake wamesha rudishwa
 
Hakuna cha UDSM wala nini sasa hivi, wote mnatoka shule hizihizi zenye kuzalisha Div. 5! Hamjitambui mkiwa chuo, hamjitambui baada ya kuhitimu...Yaani sasa kwenda chuo ni kama "fashion" wala hamuongezi kitu katika bongo zenu...ubinafsi unaongezeka, maslahi ya Taifa hakuna (Ipo siku mnaojiita wasomi wa Taifa hili mtajuta kututambua, mnatumia kodi zetu mnachofanya sufuri)
 

Vipi Steven Owawa ndo anaongoza mgomo?
 
Vipi Steven Owawa ndo anaongoza mgomo?

ha ha ha huyu jamaa aliniachiaga manyanga 2010 pale udsm kuongoza chama cha wanaharakati.... Aliingia UDSM 2005 akafukuzwa,akarudi 2006
akisimamishwa 2007 baadae akarudi,2008
akasimamishwa mwezi moja,2009
akasimamishwa mwaka mzima wakarudi baada
ya kumaliza kesi na kushinda serikali dhidi ya
viongozi wa DARUSO,na amemaliza rasmi 2010 yeye na silinde,Machibya nakumbuka hayo
machache amekuwa akifukuzwa kutokana na
msiamo mkali wa kuongoza mgomo kupinga
sera ya Uchangiaji elimu ya juu Tanzania,ni hayo
machache ninayofahamu wadau...na kwasasa yupo national audit office sijui mkoa gani ila pia kwa mbali inasemekana ni shushushu(sijathibitisha)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…