Tetesi za Makamba kuwania uenyekiti wa AU na kuwaunga mkono Gen Z kimemponza kutimuliwa uwaziri?

Tetesi za Makamba kuwania uenyekiti wa AU na kuwaunga mkono Gen Z kimemponza kutimuliwa uwaziri?

Moja ya makosa makubwa aliyofanya January Makamba ni kutaka kuwania kuwa Mwenyekiti wa African Union huku akifahamu fika kuwa nafasi hiyo inawaniwa na Raila Odinga ambaye anaungwa mkono na Rais Ruto wa Kenya.

Itakumbukwa kuwa Rais Ruto alimshawishi Odinga kuwania nafasi hiyo ili kuimarisha utawala wake ambao unatishiwa na uwepo wa Odinga kama kiongozi wa upinzani. Aidha uwepo wa Odinga ni tishio kwa Rais Ruto katika uchaguzi Mkuu ujao wa 2027 hivyo kumlazimisha Ruto kumpigia Odinga kampeni katika nchi zote za Afrika ya Mashariki kumuunga mkono. Tanzania tayari iliwisha kubali kumuunga mkono Odinga katika adhma yake ya kuwa Mwenyekiti wa AU kwa hiyo kitendo cha Makamba kutaka kuwania nafasi hiyo kinaonyesha ni utovu wa nidhamu kwa Rais Samia.

Kosa la pili la Makamba ni kuwaunga mkono Gen Z katika harakati zao za kumng'oa Rais Ruto madarakani. Makamba alionyesha kuwaunga mkono Gen alipokwenda Jijini Nairobi kuweka jiwe la msingi katika jengo la kitega uchumi la Tanzania na kushangiliwa kwa vifijo na vijana waliokuwa wanaandamana.

Makamba mara nyingi amekuwa haridhiki na nafasi anazopewa na viongozi wake wakiwemo Magufuli na sasa Samia na kutaka kuwania urais wa nchi mwenyewe.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Uzandiki, slander-mongering!
 
Kutunga ujinga nayo ni ngumu?

Tunga vitu vya maana wewe
Vitu vya maana na ujinga ni relative au mtazamo. Mtu mjinga kwake vitu vya maana ni vya kushibisha tumbo lake, nje ya hapo kwake ni ujinga!
 
Samia nina uhakika hapigi, ni wasiwasi na chuki zetu zinazotushawishi vibaya kumhusu, ni masuala ya uzanzibari wake na uislam yanayotusumbua vichwani mwetu.
Angekuwa hapigi asinge wapa ruhusa ya kula kwa urefu wa kamba!
Angekuwa hapigi asingepikika chungu kimoja na wapiga kina Mwigulu!
 
Back
Top Bottom