Tetesi za Matokeo ya NECTA kidato cha nne 2012 [Kabla Hayajatoka]

Status
Not open for further replies.
Matokeo ya kidato cha nne kwa mitihani iliyofanyika October mwaka jana yanakaribia kutoka. Katika matokeo hayo ambayo vikao vyake vya mwisho ndio vinafanyika,ufaulu umnaonekana kushuka.Nyaraka zinaonesha kuwa Shule za Seminari,kama ilivyo ada,zinaoongoza.Baadhi ya Shule za Serikali zinajikongoja ingawa ufaulu katika Shule zetu za Kata ni wa utata mtupu.

Matokeo hayo ambayo nimefanikiwa kuyachungulia kiintelijensia yanaonesha kuwa wanafunzi wa Sayansi ndio waliofaulu zaidi ya wale wa masomo ya Sanaa. Wasichana,katika ufaulu wa kitaifa,wameng'ara kuliko wavulana. Hali katika Shule zetu za Serikali hasa za Kata si nzuri hata kidogo. Yakitoka,hapatatosha!

Matokeo hayo yanatarajiwa kutangazwa muda wowote hasa kuanzia tarehe 1/2/2013.

ANGALIZO: Siwezi kutaja kwa majina Shule za kwanza na za mwisho na wanafunzi wa namna hiyo kwakuwa matokeo rasmi hutangazwa na Serikali.
 
Duu!!
Sasa kwanini serikali isiyachakachue ili ufaulu uwe wa kiwango cha kutisha kuwahi kutokea, halafu akina Kinana na Nape kule Kigoma waongeze mtaji wa kisiasa baada ya ile zuga ya kupanda treni, pia kuunadi ufaulu huo wakati wa kuomba kura 2015?
 
Kwanini una kihere*2 cha kuchungulia? Sisi tunataka matokeo rasmi bana! Kama umechungulia wrong reports je?
 
Tatizo sio kufaulu tu, wakifaulu, hakuna sehemu ya kuwapeleka........wahitimu ni wengi sana, shule za high school (serikari na private) ni chache sana

Duu!!
Sasa kwanini serikali isiyachakachue ili ufaulu uwe wa kiwango cha kutisha kuwahi kutokea, halafu akina Kinana na Nape kule Kigoma waongeze mtaji wa kisiasa baada ya ile zuga ya kupanda treni, pia kuunadi ufaulu huo wakati wa kuomba kura 2015?
 

Hiyo avatar yako ndio inaonyesha walivyokuwa wakifanya mitihani?
 
yatoke tu ili tujijue tunajipanga vipi kwenye maswala ya ada.......kama anaenda 4m5 au ndo hivyo inabidi aende certificate.
 

Na somo watakalofeli sana ni Elimu ya Dini ya Kiislamu.
 
We acha ushambenga! Ulicho andika humu hakina mantki yoyote na wala hakina msaada kwa mzazi wala mtahiniwa. Umeleta hadithi ziszo na evidence. Kama unashindwa kutaja majna ya shule kwa sabbu ni jkmu la serkali sasa kmekuwasha nn kuleta habari iso na source. Waachie NECTA wafanye kaz yao nasi tutawasikiliza ila sio habari za kilevilev. Hapa ni sehemu y watu makini tu.
 
Kwa nini hapatatosha?
 
Mhh...kweli shule zetu za kata majanga matupu! Tena baadhi ya viongoz wengi waliosoma shule kongwe za serikali na kufanikiwa tena kwa viwango vikubwa,hata hawazikumbuki shule walizo zipitia hata kuzisaidia ili ziwe na hadhi! Looh enyi watu wa namna hiyo si vizuri,hebu kumbukeni shule mlizopitia na mzisaidie!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…