PreGE2025 Tetesi za RC Kagera Fatuma Mwassa kugombea Ubunge Bukoba Mjini CCM zimeanza kuleta mgawanyiko Bukoba

PreGE2025 Tetesi za RC Kagera Fatuma Mwassa kugombea Ubunge Bukoba Mjini CCM zimeanza kuleta mgawanyiko Bukoba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkuya dr

New Member
Joined
Apr 22, 2019
Posts
2
Reaction score
0
Siasa za kuelekea katika uchaguzi mkuu kwa Bukoba mjini mkoa wa Kagera zimeingia shubiri baada ya kikao cha jana usku kutaka kuvujika baada ya RC Fatuma Mwasa kueleza adhima yake ya kugombea ubunge kupitia CCM katika jimbo la Bukoba mjini.

RC amewaeleza wajumbe kuwa ana baraka zote za viongozi wakuu japo hakuwataja kwamba ili kunusuru bukoba agombee jimbo hilo linaloongozwa na Stephen Byabato.

Katika kikao wajumbe waliomba hoja hiyo isijadliwe labda RC huyo ameitoa kama utani lakini alisisita kuwa ni uamuzi wa wakubwa.

Tangu jana katika vijiwe vya kahawa na mijadala katika jimbo hilo ni kama imegeuka gafla na wengi wameonesha kuunganisha doti na harakati za RC huyo katika jimbo hilo tofauti na maeneo mengine ambapo amekuwa akiudhuria mpaka misiba ya kwenye mitaa,sherehe za kawaida ,kutembelea vituo vya watoto,kutoa misaada na mabango mengi katika mji huo kuwekwa picha yake.

hadi sasa mji mzima umepambwa na mabango yake na Rais Samia.

Aidha RC Fatuma Mwasa tayari ameaunda Timu ya kampeini zake na watu wa habari kuhakikisha anapata kuungwa mkono na wakazi wa Bukoba.

Kumbuka RC Fatuma Mwasa ni mwenyeji na mzaliwa wa Kigoma lakini nguvu ameziwkeza Bukoba kama ilivyo kwa Makonda kule Arusha

Nitakuwa niki update habari hii juu ya kinachoendelea hadi atakapochukua fomu.

Rejea:
Mkuu wa Mkoa Kagera Bi. FATUMA agundua uozo mkubwa, Mbunge BKb Mjini na Meya wakalia kuti Kavu, waanzisha ujenzi Bila Ramani




View: https://www.youtube.com/watch?v=csgoeVk9KHs
 

Attachments

  • 789.jpg
    789.jpg
    147.7 KB · Views: 41
Ishakuwa fasheni sasa wakuu wa mikoa kugombea ubunge mikoa wanayoongoza. Arusha makonda, bukoba fatma mwassa, vipi kule njombe mtaka hataki? Halafu si ilisemwa kiongozi wa serikali akitaka ubunge aseme ili nafasi yake ijazwe fasta?
 
Back
Top Bottom