Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
Tetesi za usajili majira ya kiangazi msimu wa 2020/2021 vilabu mbalimbali vya siasa Tanzania
1. Winga teleza wa CHADEMA Saeed Kubenea amesema hana mpango wa kuhama klabu yake hiyo kuelekea klabu ya NCCR-MAGEUZI iliyomtangazia dau kubwa. Klabu ya CCM pia inamhitaji (Nipashe)
Kiungo machachari wa CHADEMA Esther Bulaya amesema kuwa hana mpango wa kurejea klabu yake ya zamani ya CCM kwani ana uhakika wa namba kwa sasa na anafurahia maisha katika klabu yake ya sasa ya CHADEMA na anaelewana vyema na kocha wa timu yake. (The Citizen)
Kiungo wa NCCR-MAGEUZI aliyekuwa na msimu mbovu mfululizo anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya CHADEMA kwa sasa, Anthony Komu amesema kuwa tayari amejiandaa na msimu ujao kutumikia klabu yake ya NCCR - MAGEUZI.(Mtanzania)
Mshambuluaji tegemeo wa klabu ya CHADEMA Peter Msigwa, anahusishwa na kuhamia katika vilabu kadhaa katika majira haya ya kiangazi. CCM pia wametupa ndoano yake. Dau limekataliwa na amesema yeye sio wa bei rahisi. Hanunuliki. (Majira)
Golikipa mashuhuri ambaye kwa sasa ni mchezaji huru Jeremia Maganja baada ya kuachana na miamba ya zambarau yenye makao yake Kijitonyama, ACT - Wazalendo, inasemekana kukaribia kusaini dili la miaka 5 kukipiga katika klabu ya CCM kwa mkopo wa muda mrefu. (Mwanahalisi Online)
Mchezaji chipukizi bora kwa msimu uliomalizika, Godlisten Malisa anaekipiga katika klabu ya CHADEMA yenye makazi yake mitaa ya Ufipa, Kinondoni ameonesha NIA ya kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Anthony Komu anaerejea katika klabu yake ya NCCR - MAGEUZI (Tanzanite)
Wakala wa mchezaji wa mkongwe wa CCM, Steven Wassira amesema anarejea rasmi katika jimbo la Bunda Mjini kuchukua nafasi ya mchezaji tegemeo wa CHADEMA, Esther Bulaya. Wakala huyo amejinasibu kwamba kwa sasa Esther Bulaya sio machachari mbele ya mchezaji wake maarufu kama 'Tyson' (Global TV)
Golikipa wa klabu ya CCM, Mwigulu Nchemba amesema nafasi yake bado ipo na hana shaka yoyote na usajili wa golikipa mwingine kutoka ACT - WAZALENDO, Kitila Mkumbo ambaye nae ameonesha NIA ya kutaka nafasi ya Mwigulu Nchemba. Kitila ni tishio kwa Mwigulu (Jamvi la habari)
Mchezaji aliyepoteza kiwango chake kwa sasa katika klabu ya CHADEMA, Joseph Selasini anatajwa kutaka kuelekea katika klabu ya NCCR-MAGEUZI baada ya kupewa ahadi ya namba. Selasini aliondolewa katika nafasi ya nahodha msaidizi na hana maelewano na kocha wake (Mwananchi)
Kiungo Machachari aliyehama kutoka klabu ya CUF kwenda klabu ya CCM, Julius Mtatiro anatajwa kutaka kupepetana na kiungo nyota wa klabu ya CHADEMA kutaka nafasi katika jimbo la Tarime mjini. Esther Matiko anatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kutetea namba yake (Millard Ayo)
Mlinzi wa CCM aliyekosa nafasi yake katika jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, ametangaza rasmi kuchuana na Mchezaji nguli wa klabu ya CHADEMA, John Heche kutaka nafasi katika jimbo la Tarime vijijini. Wakala wa Waitara amethibitisha. (Kwanza Tv)
January Makamba ameendelea kujiimarisha katika mbio zake za kutaka nafasi ya Kugombea URAIS kupitia klabu yake ya CCM. Nahodha wa timu hiyo, John Magufuli anatajwa kuwa na nguvu na ushawishi mkubwa. Makamba anasema ataendelea na nafasi yake huko Bumbuli. (Swahili times)
Sent using Jamii Forums mobile app