SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Baadhi yetu tumepiga sana kelele kuonyesha kuwa tatizo kubwa la Simba ni ukosefu wa mfumo thabiti wa uongozi unaowezesha timu kuendeshwa kwa ukaribu na umakini. Simba haina management imara, bali management ipo kama jina tu ila haina watu na waliopo hawana meno ya kutenda majukumu yao. Chukulia mfano cheo kikubwa kama cha CEO, ukiangalia mamlaka aliyonayo unaona hayaendani na cheo hicho.
Jana nimesoma Mwenyekiti wa Klabu Mangungu kamteua Kailima aliyewahi kuwa Tume ya Uchaguzi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi. Ukiachana na ukakasi kutokana na historia za utendaji wake kisiasa, Wanasimba wengi hawajawahi kumsikia huyu mtu akijishughulisha na mambo ya mpira, leo hii anapewa ujumbe wa Bodi ambayo kimsingi ndiyo inayoendesha timu.
Wajumbe wengi walioteuliwa na pande zote mbili hata wale waliojiuzulu wana majukumu mengi ya Kiserikali. Hata kama wanaweza kuwa na mapenzi na Simba, nina uhakika ni kazi sana kuwakutanisha hawa watu kutokana na muingiliano wa ratiba zao. Muda wanapata wapi hawa kushughulikia mambo ya mipira? Simba haitakiwi kuwa "pet project" ya Mo, Mangungu wala Wajumbe wa Bodi, inatakiwa kuwa kipaumbele chao wanapoamka hadi wanapolala.
Simba inatakiwa kupanua na kuimarisha Timu yake ya Management, iwe na idara za kutosha na Wakurugenzi wa Idara hizo ndiyo waunde Bodi ya Wakurugenzi. Hawa Wakurugenzi wawe waajiriwa rasmi wa Simba na wapatikane kwa kupitia mchakato rasmi wa ajira na wafanye kazi full time katika idara zao.
Hawa wanasiasa wanaoteuliwa wapelekwe huko kwenye Friends of Simba au ile Executive Network au Baraza la Ushauri. Timu imekuwa na muundo wa ajabu ajabu ndiyo maana kila mtu amekuwa kambale.