Nachukua nafasi kumwomba Waziri wa Habari Na michezo Mh.Nape aiingilie kati tabia ya TFF kuingilia chaguzi zinazifanywa Na vilabu hapa nchini.TFF iliyumbisha uchaguzi wa klabu ya Simba, TFF iliingia katika mgogoro Mkubwa Na klabu ya Yanga wakati wa uchaguzi, TFF ilivuruga chaguzi za vilabu vya Coastal Union Na African Sports za Tanga Na mwisho tumeiona TFF ikiingilia uchaguzi wa Stand United Na kupelekea Mahakama kuingilia kati Na kuufuta uchaguzi ulioingiliwa Na TFF.Tunakuomba Mh.Waziri ikomeshe tabia hii ya TFF kwani inazorotesha michezo nchini.