TFF acheni kuingilia chaguzi za vilabu, mnaleta migogoro

TFF acheni kuingilia chaguzi za vilabu, mnaleta migogoro

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
2,282
Reaction score
1,252
Nachukua nafasi kumwomba Waziri wa Habari Na michezo Mh.Nape aiingilie kati tabia ya TFF kuingilia chaguzi zinazifanywa Na vilabu hapa nchini.TFF iliyumbisha uchaguzi wa klabu ya Simba, TFF iliingia katika mgogoro Mkubwa Na klabu ya Yanga wakati wa uchaguzi, TFF ilivuruga chaguzi za vilabu vya Coastal Union Na African Sports za Tanga Na mwisho tumeiona TFF ikiingilia uchaguzi wa Stand United Na kupelekea Mahakama kuingilia kati Na kuufuta uchaguzi ulioingiliwa Na TFF.Tunakuomba Mh.Waziri ikomeshe tabia hii ya TFF kwani inazorotesha michezo nchini.
 
Malinzi mwaka huu anapumulia mashine. Haya leo mahakama imembamiza mpambe wake. Safi sana mr. Amani mwenyekiti wa standi united kwa kumchanachana malinzi na kitff chake.

Timu dokodoko kamueni mpaka mifupa.
Ndimbo, Msabaha, Koto na Mwakasungura. Nawasalimu.
 
Back
Top Bottom