TFF anzisheni Leseni ya uchambuzi WA soka.

TFF anzisheni Leseni ya uchambuzi WA soka.

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Kwa Hali ilivyo Sasa, Mtu anatoka baa anapitia studio anahojiwa eti ni Mchambuzi wa soka inafubaza ubora WA soka la Tanzania.
Kama mawakala wa Wachezaji Wana Leseni na wanafanya mitihani kabla ya kuzipata iweje kuchambua soka ambako kunahitaji utaalamu zaidi iwe holela? Mtu aliyefeli kwenye Uwakala wa Wachezaji anakimbilia kuwa mchambuzi uchwara na Hakuna cha kufanya maana Hakuna sheria inayombana.
Ni wakati Sasa nchi iwe na Kanuni mahususi zinazosimamia tasnia hii adhimu ya uchambuzi na kama Mtu anaitwa siyo mchambuzi mwenye kutambulika chombo cha habari kilochomuita kiseme Wazi huyu tumemuita kama mchezaji wa zamani au shabiki tu.
 
"Tunataka kuona katika Taifa hili, vijana jeuri na wenye kujiamini, si vijana waoga, akina "ndiyo bwana mkubwa", vijana wanaohoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa"

Mwl J.K. Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania
 
Back
Top Bottom