TFF fanyieni kazi wazo la Rais Magufuli kuwaweka wachezaji kutoka majeshi

ware makomando wanaopasua tofali kwa kichwa ukiwapa mpira kipa akidaka kiki yao anakufa hapo hapo
 
Mkuu unamaanisha jeshi lipi?
Kwani kwenye michuano ya ligi kuu Tanzania si kuna timu za majeshi,
ni ipi kati ya hizo inaongoza ligi? au
kuweka wanajeshi hakumaanishi kuifanya timu icheze vizuri na kushinda?
 
Nchi zenye vita zimeisha? Mpira sio ubabe unaweza shangaa siku ya game vinapaki vifaru na Ak47 za kutosha.
 
Ivi ni yeye au kuna mtu anatucheza shere pale maeneo, mbona kauli zinamsaliti sana?[emoji2] [emoji2]
 
Kwani nchi zenye vita zimeisha?? wanajeshi sio lazima kila kitu wao
 
Mmeanza kutaka kumpangia na kumuingilia Kocha. Acheni porojo. Kama kocha ataona kuna kifaa bora kabisa kutoka Jeshini, awe huru kuchagua. Timu nyingi huvurunda huko AFCON baada ya wanasiasa kujipenyeza kwenye team selection
 
Timu za jeshi zipo nyingi tuu daraja la kwanza mbona hazifanyi vizuri kwani Nchi zilizoendelea kisoka Timu zao ni za jeshi? au maendeleo na jeshi kuna uhusiano gani mawazo ya kawaida sana hayo ingawaje yupo na vijana vizuri mengine tuyaache tu.
 
Jkt Tanzania,Mlale jkt,Orjoro Jkt,Tanzania prisons,Ruvu shooting,Police Tanzania......hizo timu zimefanya jipya gani Tz?
 
Nadhani hii ni lack of knowledge jinsi mpira unavyoendeshwa...., hii ni Timu ya Taifa..., yoyote mwenye uwezo anaweza kuchaguliwa na sababu ya exposure na ugumu wa ligi kuu katika nchi, basi naturally wachezaji wengi wazuri wanapatikana katika ligi hii ndio maana asilimia kubwa wanatoka kwenye ligi..., kama mjeshi ni mzuri hata akiwa mafichoni basi timu yoyote kubwa katika hii ligi kubwa itamuona na hence mwisho wa siku atakuwa Timu ya Taifa...

Kama issue ni kukosa ukakamavu basi wachague mtu wa kuwapa mazoezi mjeshi au waende field jeshini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…