TFF hakikisheni ahadi ya pesa kwa Timu iambatane na wajibu

TFF hakikisheni ahadi ya pesa kwa Timu iambatane na wajibu

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Binaadamu ukimuahidi au akitarajia jambo anaweza asijali sana usalama wa wengine na wakati mwingine hata usalama wake mwenyewe.

Teja anapohitaji pesa au chochote ulichonacho haoni shida kukuchoma kisu au bisbisi ya ubavu...kwake kwa wakati huo chenye thamani ni elfu mbili uliyonayo na sio uhai wako.

Niwapongeze Silent Ocean kwa motisha wanayoitangaza kwa Timu wanayoidhamini, na tena ni jambo zuri kuwa wanaweka mambo hadharani badala ya kama wangefanya tu kwa siri.

Ila sasa ningeshauri kwa TFF kuweka utaratibu ambapo hizi ahadi ziende sambamba na kuwasihi Waahidiwa kuwa wacheze kiungwana (fair play), na iwapo mechi itaisha huku wamewaumiza wenzao kwa mchezo usio wa kiungwana basi wanaweza kukosa au kupunguza hicho walichoahidiwa.

Kuna faida gani kwa Mdhamini anayetoa ahadi iwapo timu yake hiyo itashinda na kuwaacha Wachezaji wenzao Majeruhi hata kama wameshinda?.

Hivyo isitoshe tu kuwaambia Timu mkishinda tutawapa kiasi kadhaa na kuwaacha tu wafanye vyovyote wawezavyo washinde.

Kuwe pia na vigezo na masharti.
 
Wanaotoa ahadi wawe wanapeleka hela TFF, ahadi ikisababisha madhara TFF ikate kufidia gharama za madhara
Natania tu
 
Back
Top Bottom