Wenye Akili Kubwa mnatushangaza sana yaani Matukio mengine mnayatolea Matamko upesi sana ila sijui kwanini hili la GSM Kujitoa katika Udhamini Mwenza wa Ligi Kuu ya NBC nanyi kama TFF mnachelewa kulitole Tamko wakati Wao ( GSM ) walishatoa lao na tumewaelewa kwa Kiasi chao.
au mnaogopa Kuwajibu ( kutoa Tamko ) Kuwajibu kwakuwa mnajua baadhi yenu mtaumbuka kwani pamoja na kwamba mpaka Udhamini wao Ulisainiwa hadi hivi juzi walipojitoa Vilabu havikupata Fedha zao ila nyie Waandamizi Watano ( nawahifadhi ) wa TFF mmekuwa mkipokea mno Pesa zao Kinyume na Utaratibu?
Tuliwaonya mapema kuhusu GSM ila mkatuona hatunazo ( Mazuzu ) na baada ya kujua Udhaifu wenu wa Tamaa na Upigaji hapo TFF jamaa ( GSM ) wakatumia Akili Kubwa Kuwarubuni ili muwakubali kisha mkiwa nao wawafanyie Umafia huo, wawasome, wajue Siri zenu na wakijotoa waanze kuanika Hadharani Madudu kusudi Mkakati wao wa Kuwachafua kwa Jamii ( Public ) ukamilike na umeshakamilika.
Na nasikia Watu wa GSM wanasubiri kwa hamu zote reaction ( response ) yenu kuhusiana na kule ( huko ) kujitoa Kwao kama Mdhamini Mwenza wa NBC Premier League ili kama nanyi mkiwajibu kwa Kuwasema, Kuwalaumu na Kuwashutumu basi na Wao warejee na Bomu lenu la mwisho ambalo naambiwa litawaacheni Uchi TFF nzima na Wadau ( Wananchi ) hawatowaelewa na huenda hata ukaathiri Udhamini huu Mkuu wa NBC.
TFF mmeshikwa patamu sana na GSM.