TFF ichunguzwe TAKUKURU wapo

TFF ichunguzwe TAKUKURU wapo

nditolo

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
3,731
Reaction score
4,271
Hili suala la mikataba mibovu mda mrefu imekuwa ikisababisha umasikini, mauwaji na hasara mbalimbali kwa jamii hapa Tanzania . Huko serikalini ni kugumu kidogo lkn kwa Hawa TFF na bodi ya league Kuna umuhimu mkubwa wa kuwachunguza. Wanahujumu team.

Imagine unataka biashara itangazwe kwa milioni tatu tu ndani na nje ya nchi kwa team Kama Simba sc?

Tusingekuwa na Yule dada imara pale Simba Mambo yangekuwa sio kabisa.

League yetu wanataka iwe utopolo tu.

Wachunguzwe na wawajibishwe. Hatutakibali upuuzi huu.
 
Hoja ya msingi sana, inaonekana kuna baadhi ya viongozi wa TFF na bodi ya ligi wako kwenye payroll ya GSM, kitendo walichomfanyia Barbara leo kumzuia kuingia uwanjani naona ni hasira zao kuharibiwa dili lao na GSM, ndio maana hawakutaka ule mkataba ujadiliwe, ni wahuni.
 
Angalia tu chaguzi zao sio wazi.

Na Yule kasongo aliingiaje pale bodi ya ligi kwa sifa zipi?
 
Huyo Kasongo ndio waanze nae, juzi nimemsikia akijitetea kwanini hawakutaka ule mkataba wao na GSM ujadiliwe na vilabu, anadai walikuwa na haraka hawakupata muda wa kuvishirikisha vilabu, nikajiuliza hiyo haraka ya nini? jamaa ni wajanja janja wako rahisi sana kuwa corrupted na GSM.
 
Yaani kwa takriban miaka5 tff hiyo hiyo imekuwa ikiwabeba kwambeleko tena ya chuma nyie makoloa, leo hii mnataka wachunguzwe??
 
Okay tumepata pa kuanzia. Yaani hawakupata muda wa kushirikisha vilabu. Je kulikuwa na uharaka gani?

Na wao ni nani mpaka wakae waviamulie vilabu.

Na aseme hiyo ten % aliyosaini kwa niaba ya vilabu alikula Bei gani
 
Yaani kwa takriban miaka5 tff hiyo hiyo imekuwa ikiwabeba kwambeleko tena ya chuma nyie makoloa, leo hii mnataka wachunguzwe??
Hata malinzi tulinfunga baada ya kuwabeba utopwinyo
 
Hii hoja tumechoka kuijadili kwani hakuna point na evidence zozote ni umbea na unoko
 
Hili suala la mikataba mibovu mda mrefu imekuwa ikisababisha umasikini, mauwaji na hasara mbalimbali kwa jamii hapa Tanzania . Huko serikalini ni kugumu kidogo lkn kwa Hawa TFF na bodi ya league Kuna umuhimu mkubwa wa kuwachunguza. Wanahujumu team.

Imagine unataka biashara itangazwe kwa milioni tatu tu ndani na nje ya nchi kwa team Kama Simba sc?

Tusingekuwa na Yule dada imara pale Simba Mambo yangekuwa sio kabisa.

League yetu wanataka iwe utopolo tu.

Wachunguzwe na wawajibishwe. Hatutakibali upuuzi huu.
Misimu yote minne iliyopita hamkuyaona hayo?
Kwani Yanga hawakulalamika na mkawacheka?
Na nyinyi tulieni kimya msitusumbue.
 
Hoja ya msingi sana, inaonekana kuna baadhi ya viongozi wa TFF na bodi ya ligi wako kwenye payroll ya GSM, kitendo walichomfanyia Barbara leo kumzuia kuingia uwanjani naona ni hasira zao kuharibiwa dili lao na GSM, ndio maana hawakutaka ule mkataba ujadiliwe, ni wahuni.
Umebeba kadi imeandikwa watoto hawaruhusiwi unafosi uingie na watoto majina yalioandikwa kwenye kadi sio ya watoto ulioambatana nao unataka TAKUKURU waichunguze TFF badala ya kuomba kumchunguza huyo CEO wa Simba alivyotaka kutumia madaraka yake vibaya kuingia uwanjani na watoto ambao hawaruhusiwi kuingia VVIP. Omba TAKUKURU wamchunguze Babra kama alitumia madaraka yake vibaya ya uceo wa Simba kulazimisha kuingia na watoto ili Sheria ifuate mkondo wake.
 
Back
Top Bottom