Mechi ya jana walikutana wote wacheza mieleka wanaotumia mpira.
Kuna wahuni wanaoharibu mchezo wa soka hapa nchini linapokuja suala la anga kubebwa na waamuzi unawaona wanajitahidi kuleta hoja kana kwamba eti ni mambo ya kawaida tuyazoee.
Hata hoja ya milioni 40 wanajitahidi kuipuuza na kumlaumu aliyeisema wazi wazi. Jambo la kushangaza ni pale kipa mmoja aliyewahi kuituhumu Simba kuwa ilitaka kumhonga gari, aliitwa kwenye kituo chao na akapewa karibu ya saa nzima kumiliki kipindi na kuwaelezea umbea huo uliokuwa na lengo la kuichafua tu brand ya Simba. Hakuwa na ushahidi. Huyu mwenye ushahidi wa simu kupigwa, anapuuzwa na kutakiwa aadhibiwe yeye kwa kusema ukweli.
Kuna siku mtapata mkitakacho.