TFF inapaswa kumchukulia hatua zaidi mchezaji wa Tanzania Prison aliyetolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Simba

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Nimerudia kuangalia tena rafu ile ya kishamba aliyocheza yule mchezaji, nimejiridhisha kwamba kadi nyekundu pekee haitoshi , yule mchezaji anastahili adhabu zaidi, ikibidi hata kufungiwa michezo kadhaa.

Hili likifanyika litaongeza nidhamu kwa wachezaji wengine, haiwezekani tukaacha wachezaji wacheze kijinga vile kisa wanatokea kwenye timu za Majeshi , soka na gwaride au Parade za maadhimisho fulani havifungamani.
 
Bora wasichukue hatua yoyote kwani matukio kama hayo ndio yanaifanya ligi kuu ionekane maarufu Afrika Mashariki

Alisikika mlevi mmoja
 
Kuna kipindi kuna beki wa timu moja ya majeshi alimchezea sana rafu Tambwe wakati yuko Simba utopolo walishangilia ila msimu uliofuata wakati Tambwe kahamia yanga beki yuleyule akamchezea Tambwe kihuni ila safari hiyo kwa sababu alikuwa utopolo wakapiga sana kelele za kulalamika kwa maoni uliyotoa na maelezo ya Eymael sishangai na bahati nzuri mnakutana nao kombe la shirikisho
 
Umeandika unyama sana !
 
Hahahah utopolo bana!!!
 
Kunamambo yanawapata Simba,Utopolo wanafurahi ilhali Simba wametulia na awajapanic.
Ngoja sasa Utopolo wakutane na wao na izo changamoto kama za Simba. wataita press kulaumu bodi ya ligi,tff,Manara na MO.
 
Droo imewaumiza sana mikia,mshukuru ile mbeleko la sivyo maumivu yangekua makali zaidi
 
Sisi Simba SC tunapokutana na Changamoto mchezoni huwa tunamlaumu mchezaji husika but wenzetu Utopolo wanapokutana na Changamoto kama hizi wanawalaumu Marefa, TFF, Bodi ya Ligi na Serikali.
 
Sisi Simba SC tunapokutana na Changamoto mchezoni huwa tunamlaumu mchezaji husika but wenzetu Utopolo wanaikutana na Changamoto kama hizi wanawalaumu Marefa, TFF, Bodi ya Ligi na Serikali.
Ndo kawaida yao kulia lia na kupigia kelele hata wasiohusika ref..Vyura kwenye vidimbwi vyao yani ni kelele mtindo mmoja kweli jina la Vyura linawafaa utopolo.
 
Kufungiwa kwa mchezaji kwetu huku haiwezi kumbadilisha mchezaji,kwani wengi wana attitude za ajabu sana.

Inatakiwa watu kama hao wapigwe faini kubwa kuanzia laki 5
 
Duh kuna watu sijui kama ubongo umo ama umeshaliwa na kamasi tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…