TFF inavuna ilichopanda kwenye mpira

TFF inavuna ilichopanda kwenye mpira

Huna unachokijua wewe, huko uingereza timu zinaigomea FA mara kibao. Kipindi Newcastle inataka kununuliwa na Bin Salman timu ziligoma na FA ikanywea na kusitisha ununuzi wake kwa muda hadi uchunguzi ufanyike. La Liga mwaka juzi kama sikosei ilitaka kuingia mkataba na kampuni ya kimarekani ili baadhi ya mechi zikachezwe US, timu zikaukataa. Na juzi tu, Real Madrid, Barcelona na Athletic Bilbao zimegomea mkataba baina ya laliga na kampuni ya CVC, wanatarajia kufhngua kesi. Kwahiyo kama wewe ni mbumbumbu, baki na umbumbumbu wako, usilazimishe wengine waungane na wewe.
Hizo ni timu na sio timu moja. Yaani, timu zooooooote kwenye ligi zinasema sawa ispokuwa timu moja tu. Hivi hiyo timu moja inayosema hapana ingekuwa ni Ihefu TFF ingeondoa mabango ya GSM au ingegomea rangi ya nembo ya mdhamini?. Umeongea utumbo mbichi wewe. Ondoa mahaba yako ili uusaidie mpira.
 
Ona hapa, Barbara kaalikwa yeye VVIP kama Barbara CEO wa Simba anaamua kusomba watoto na mashemeji kwenda nao VVIP, kama sio ushamba ni nini, kama sio kiburi cha kuiweka TFF mkoni ni nini? Kama sio kujiona na fedha za mo ni nini?. Yaani unamwalika demu wako dinner sehemu fulani halafu demu wako anakuja na rafiki zake bila kukutaarifu mapema ili useme YES or NO kulingana na bajeti yako, meza na viti vya kutosha viandaliwe, malazi na glasi za kutosha vitayarishwe, nk. Huu ni uhuni sawa na uhuni mwingine tu kwenye mpira, mbwa anawafuata hata msikitini TFF watulie tu. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
 
Mimi ni mpenda mpira tu nchini, sijali sana usimba na uyanga. Eti nchi ndogo kama hii TFF inaruhusu wachezaji 12 wa kigeni kila timu. Yaani 12x16 . ligi imejaa wacongo
Kati ya hizo timu 16, ni ngapi zenye wachezaji wa kigeni 12?
 
Suala la mkataba wa TFF na GSM hakuna duniani suala kama hilo, GSM anaizamini Yanga, na timu zingine 2 ndani ya ligi moja halikubaliki ni mgongano wa maslahi ni hapo match fixing inaweza tokea, hafu tena GSM anataka kuzamini ligi hapo haiko sawa kabisa kama anataka azamini ligi ajitoe kuzamimlni vilabu
League ya South Africa ina dhaminiwa na DStv ambao ni wamiliki wa Supersport Utd na hakuna kelele hivi sisi bongo tuna cheza mpira upi? niambie kwa details udhamini wa GSM unawanfuaishaje Yanga wakati tumeona mechi ya Namungo na Yanga ilovyokua tight?
 
Kati ya hizo timu 16, ni ngapi zenye wachezaji wa kigeni 12?
Ni uwezo wa kifedha tu timu nyingine zinaukosa wa kusajili wachezaji wageni 12. Ndiyo maana TFF inatafuta wadhamini wengi kadiri inavyowezekana ili timu zote angalau ziwe na uwiano mzuri wa kifedha na kusajili. Ona sasa timu kubwa zenye fedha zinafanya jitihada kuizuia TFF kupata wadhamini kama GSM kwa sababu ambazo hazina mashiko wala kufanyiwa utafiti. Hivi timu ikidhaminiwa na GSM itakubali ifungwe hovyo ili izikose pesa za Azam na matangazo? itakubali ifungwe ili isiwe bingwa?, itakubali ifungwe hovyo na timu nyingine ili isishiriki mashindano ya CECAFA na CAF? Kuwaza kama hivi ni dharau kubwa kwa TFF na timu nyingine kwenye ligi zikiwemo Azam na timu za majeshi kwenye ligi. Anaewaza hivyo amewaza hovyo. TFF isimame kwenye nafasi yake badala ya kupepesa macho kwa timu zenye majina, timu ndogo zinawekeza lakini TFF inazikatisha tamaa kwa kuzikumbatia Simba na Yanga.
 
Back
Top Bottom