TFF inazipendelea Simba na Yanga na kuzisahau timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu

jpak

New Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
2
Reaction score
3
Inasikitisha sana kuona shirikisho la soka Tanzania TFF eti wanaahirisha mechi za ligi kuu kwaajili ya kuwapa muda wa kujiandaa Simba na Yanga, ni kichekesho sana.

Hii inaonesha kwamba TFF wameifanya ligi ya Tanzania kuwa ni ligi ya timu mbili tu, wengine ni wapambe tu!! Pia eti kama Simba anacheza leo basi Yanga atacheza kesho hata kama wanacheza mikoani, sasa najiuliza wanini wasicheze siku moja kwani wao ni akina nani?

Hebu tuache mambo ya kubabaisha!! Simba na Yanga ni timu za kawaida tu kama Ndanda au Stand United.

Naomba TFF waache ubaguzi na haki iwe sawa kwa timu zote zinazoshirki ligi. Hii hali ya upendeleo kwa Simba na Yanga ndiyo inayolifanya soka la Tanzania lishindwe kupenya anga za kimataifa, tutaishia kushabikia Simba na Yanga tu lakini kimataifa tutaishia kushabikia timu za wenzetu.
 
Mkuu hujui hilo? Sio TFF pekee bali hata baadhi ya viongozi wako Simba na Yanga tu! Unakuta mkuu wa mkoa flani siku timu ya mkoa anaouongoza inacheza either na Yanga au Simba basi ye atashabikia moja kati ya timu hizo kongwe!!
 
New Member Jifunze kuandikia kwa Aya, ili uzi wako uvutie.. Hapo wasomaji wataona Madudu tu!.. Karibu JF!
 
Ila ameelweka na kimsingi mada yake INA logic, hata ligi za wenzetu hakuna kuahirisha mechi kwa sababu kama hizi za tff, wabadilike ili kuimarisha soka letu.
New Member Jifunze kuandikia kwa Aya, ili uzi wako uvutie.. Hapo wasomaji wataona Madudu tu!.. Karibu JF!
 
UNAJUA BODI IKONAKINA NANI WALAUSINGEPOTEZA HUUMDA HAPA
 
Ila ameelweka na kimsingi mada yake INA logic, hata ligi za wenzetu hakuna kuahirisha mechi kwa sababu kama hizi za tff, wabadilike ili kuimarisha soka letu.
Amegusia Kitu cha Msingi kwa kweliii!
 
Mwenyewe nilistaajabu sana mkuu, ndio maana soka la bongo haliendelei. Usanii mwingi sana.

Mijitu mizima inakaa kikao eti mechi za katikati ya wiki Simba na Yanga ziahirishwe ili kuwapa muda wa kujiandaa na derby yao ya kipuuzi. TFF ni mbweha kabisa. Kama mnawaona wa muhimu sana basi wahamishieni kwenye ligi ya Dar.
 
Hiyo ni kasumba.

Usipokuwa Simba au Yanga utakuwa timu gani?

Hata kama upo Mbao FC,ila lazima utakuwa Simba au Yanga.
 
Hiyo ni kasumba.

Usipokuwa Simba au Yanga utakuwa timu gani?

Hata kama upo Mbao FC,ila lazima utakuwa Simba au Yanga.
Jisemee mwenyewe, mbona mimi nashabikia Kagera Sugar tokea kitambo na sina mapenzi yoyote kwa Simba wala Yanga!
 
kibongo bongo soka ni simba au yanga......

achana na viongozi..... unakuta mtibwa na yanga inacheza lakini kuna mchezaji anayecheza mtibwa lakini ni shabiki wa yanga......

khs kutocheza cku moja simba na yanga nadhan ni sababu za kibiashara na ratiba za kuzionyesha hzo mechi kutoka azam media.....
 
Nimekuwa nikijuiliza swali na namna hii kwa miaka 10 hadi kufikia weekend iliyopita.
Sikuwahi kuona Yanga na Simba wakicheza siku moja iwe mikoani au popote. Swali langu lilikuwa moja tu TFF WANA LENGO GANI?
Nilishangaa sana kusikia kwamba TFF wanataka kubadili ratiba wiki iliyopita ili Simba na Yanga wasogezewe mechi mbele ili wapate muda wa kujiandaa kwa derby!! Nikajiuliza derby ni fainali???
TFF ndio mchawi wa mpira Tz, hakuna mwingine na wala asitafutwe popote, ila TFF TU
 
Write your reply...TFF ndiyo sumu ya mpira wa nchi hii..jana wamejazana milangoni kukusanya mapato
 
Haya mambo ni ya ajabu kabisa, kuna timu Leo zimecheza mechi ya nane tangu ligi imeanza yanga ana 5 na atakuja kucheza game ya sita hadi tar 7 simba mambo ni hayo hayo.
Hakuna soka litakua kwa kuongozwa hivyo.
Wao wanachotaka bingwa awe kati ya simba au yanga. Mwakaa huu hata mbao angeweza kuwa bingwa ila amebananishiwa game hadi kupua ni shida.
 
Arsenal alicheza na CITY na CHELSEA mfululizo.... sisi huku tunaahirisha mechi za watani ili watani wakikutana wawe na pumzi! Yanga anaenda Morogoro kumuwinda mnyama.... Juzi Real na Atletico wamekipiga na wote walikuwa pale pale Madrid
 
unapoongelea simba na yanga nchi hii dhidi ya timu pinzani ni sawa na kuongelea ccm dhidi ya vyama vya upinzani sidhani kama yataisha
 
Mpira wa Bongo ni upuuzi mtupu,tutabaki kuwa wasindikizaji maisha.Nashangaa kuna watu wanaamini Stars inaenda AFCON mwakani kwa mipango ipo na kujiandaa kupi?
 
Bila Simba sports clab ligi ya bongo itakuwa sawa ligi ya Zenji, lazima iheshimiwe
 
Kuhusu mechi kuhairishwa ..Simba ndio waliandika barua TFF maana wanajuwa kikosi chao wamejaa wazee hawawezi kucheza mfululizo...Yanga walikataa mechi yao kuhairishwa...
 
Mkuu naunga mkono hoja kua timu zote zinahitaji same treatment toka TFF. But umefanya kosa kubwa, kumfananisha bingwa mtetezi wa TPL, na timu kama Ndanda na Stand. Inabidi ututake radhi Simba SC. Levo zetu kwa sasa ni Esperance, TP Mazembe, Al Ahly, Mamelod Sundowns n.k
Kuhusu Yanga sina neno. Levo zake ndo hao hao kina Stand, Ndanda, Alliance n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…