Inasikitisha sana kuona shirikisho la soka Tanzania TFF eti wanaahirisha mechi za ligi kuu kwaajili ya kuwapa muda wa kujiandaa Simba na Yanga, ni kichekesho sana.
Hii inaonesha kwamba TFF wameifanya ligi ya Tanzania kuwa ni ligi ya timu mbili tu, wengine ni wapambe tu!! Pia eti kama Simba anacheza leo basi Yanga atacheza kesho hata kama wanacheza mikoani, sasa najiuliza wanini wasicheze siku moja kwani wao ni akina nani?
Hebu tuache mambo ya kubabaisha!! Simba na Yanga ni timu za kawaida tu kama Ndanda au Stand United.
Naomba TFF waache ubaguzi na haki iwe sawa kwa timu zote zinazoshirki ligi. Hii hali ya upendeleo kwa Simba na Yanga ndiyo inayolifanya soka la Tanzania lishindwe kupenya anga za kimataifa, tutaishia kushabikia Simba na Yanga tu lakini kimataifa tutaishia kushabikia timu za wenzetu.