TFF iongeze idadi ya wachezaji wa nje ili kukuza soka letu

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Inapaswa TFF ikubaliane na maombi ya vilabu vya Azam, Simba na Yanga ya kuongeza idadi ya wachezaji wa nje kufikia kumi. Mie nakubaliana na vilabu hivo kwa asilimia mia moja. Ukichunguza nchi ambazo zimepiga hatua kwenye soka ni pamoja na kuruhusu wachezaji wa kigeni.

Nchi yetu sio kama Ujerumani na suala la kusajiri unategemea uwezo wa vilabu. Mfano ni nchi za Ulaya na UEFA ilichofanya ni kuhakikisha mchezaji yoyote bora hapa duniani anakwenda huko kwa vyovyote vile.

Simba, Yanga na Azam wanauwezo wa kusajiri wachezaji wa kigeni hivo kwa kufanya hivo (wakiruhusiwa) watawapa moyo wachezaji wetu wa hapa nchini kujituma kupambana nao. Mfano Yanga iwe na walinzi toka nje halafu inakutana na JKT Ruvu ambayo itakuwa na washambuliaji wazawa na Yanga kufungwa patakuwa na ushindani mkubwa na vilevile kuwapa uwezo wachezaji wetu wa kujiamini.

Ila kama tutabaki na kasumba hii hii ya kutegemea timu yetu ya taifa ijazwe na wachezaji toka Yanga, Simba na Azam tu HATUTOKI!
 
Naunga mkono
Ndio mkuu. Sio timu zote zinauwezo wa kusajiri wachezaji wote kumi wa nje, hivo timu ya taifa itaundwa na wachezaji toka timu hizo kujazilizia na hao wa Yanga, Simba na Azam.
 
Wachezaji wa bongo ni wazembe,inatakiwa waletwe wengi wa nje ndo tutajifunza
 
Binafsi sioni njia hiyo kuwa kama kigezo pekee muhimu cha kukuza soka la Tanzania, kwa kuongeza idadi ya wachezaji

kutoka nje.

Mkazo uwe kuibua vipaji vya wachezaji toka wakiwa wadogo, kwa mfano kwa kupitia "soccer development academy"

kwa kuanzia zinaweza kuwa katika kila wilaya, mkoa, kanda hadi ngazi ya taifa.

Timu kadhaa zingepata urahisi wa ku "scout" wachezaji wanaowahitaji kupitia vituo hivyo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…