Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,703
- 1,724
Inapaswa TFF ikubaliane na maombi ya vilabu vya Azam, Simba na Yanga ya kuongeza idadi ya wachezaji wa nje kufikia kumi. Mie nakubaliana na vilabu hivo kwa asilimia mia moja. Ukichunguza nchi ambazo zimepiga hatua kwenye soka ni pamoja na kuruhusu wachezaji wa kigeni.
Nchi yetu sio kama Ujerumani na suala la kusajiri unategemea uwezo wa vilabu. Mfano ni nchi za Ulaya na UEFA ilichofanya ni kuhakikisha mchezaji yoyote bora hapa duniani anakwenda huko kwa vyovyote vile.
Simba, Yanga na Azam wanauwezo wa kusajiri wachezaji wa kigeni hivo kwa kufanya hivo (wakiruhusiwa) watawapa moyo wachezaji wetu wa hapa nchini kujituma kupambana nao. Mfano Yanga iwe na walinzi toka nje halafu inakutana na JKT Ruvu ambayo itakuwa na washambuliaji wazawa na Yanga kufungwa patakuwa na ushindani mkubwa na vilevile kuwapa uwezo wachezaji wetu wa kujiamini.
Ila kama tutabaki na kasumba hii hii ya kutegemea timu yetu ya taifa ijazwe na wachezaji toka Yanga, Simba na Azam tu HATUTOKI!