TFF iwaandikie barua CAF kupinga kuchezeshwa mechi zetu za Afcon qualifier na waamuzi wabovu

TFF iwaandikie barua CAF kupinga kuchezeshwa mechi zetu za Afcon qualifier na waamuzi wabovu

Moshi25

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,555
Reaction score
4,118
Kitendo cha mpira wa adhabu ndogo waliopata Niger kupigwa juu sana na bila kuguswa na mchezaji yoyote na ukatoka nje na kwa maajabu ya kila alietazama mechi ya Niger na Tanzania na Niger kupewa kona kimetia aibu mno waamuzi wapumbavu wa kiafrika wanaobeba timu zao bila aibu.

Leo kila mchezaji wa Niger alijua refa ni wao na walijiangusha mara 1000 na kupewa faulo 1000. Jambo hili liliwatoa mchezoni kabisa Taifa Stars wote hasa Tshabalala, Manula, Job, Msuva na Samatta ambao walimuwakia mno refarii.

Haji Mnoga alifanya tackling na akaupiga mpira akishindana na mchezaji wa Niger ila cha ajabu akapewa kadi ya njano je refarii alitumia sheria namba ngapi?

Wachezaji wa Taifa Stars waliangushwa mara nyingi na refa alipeta tu ila hakupeta kwa Niger aliowatengenezea faulo nyingi nje ya box ili watufunge na wakashindwa!

Mimi kama mpenzi wa timu yetu ya Taifa naomba TFF waangalie tena mechi kisha watume barua CAF kulalamika uchezeshwaji mbaya na wenye upendeleo wa wazi wa mechi ya Taifa Stars na Niger.

Tusipolalamika CAF kuhusu waamuzi , jamaa watatugeuza maboya wa kundi na watatunyonga sana kila mechi maana mechi ya upande mmoja imeisha Algeria 2 Uganda 0 sasa tayari tumeanza vizuri kampeni ya kwenda Ivory Coast maana nimetazama mechi yote Uganda wachovu tu.

Kim alipaswa kumuanzisha Sureboy badala ya Himid Mao.Sureboy yuko kwenye kiwango kikubwa kwa sasa na ana mpira wa kasi na angeiunganisha timu kutoka katikati na wale wa mbele na angepeleka mbele mashambulizi . mechi ya Algeria aanze please ili achezeshane na Feisal,Msuva,Samatta na Mpole au Kibu

Mzamiru alitimiza kikamilifu majukumu yake ya kukaba na kusaidia kwa kiwango cha juu kuzuia tusifungwe goli la pili ila alikuwa mzito sana na hakuharakisha kupeleka mpira mbele pale tulipokuwa tukishambulia hasa kumpa mpira Kibwana alipokuwa tayari ameanza marathon zake!

Kibu Denis alicheza vizuri mno na kuwakosesha utulivu kabisa mabeki wa Niger ila hakupata usaidizi wa Msuva, Samatta na Feisal. Inafaa aingie kipindi cha pili kama mechi ya jana wapinzani wetu wakiwa wamechoka na achezeshane kampa kampa tena na Msuva, Feisal na Samatta sio kupambana binafsi.

Samatta alicheza vizuri sana akionesha ni high class player na kufanikiwa kuwajengea kujiamini wale aliowaongoza uwanjani na akaweza kupiga kichwa safi cha kideoni japo mpira ulitoka sentimita chache kutoka goli la Niger ila kuna makosa alifanya mara kadhaa ya kutaka kupiga chenga timu nzima ya Niger yakaigharimu timu pale aliponyang'anywa mpira. Pia awasaidie wenzake kukaba tunapokuwa tumepoteza mpira.Huyu bado ni mchezaji tegemeo wa Taifa Stars na wa kujivunia kwa miaka kadhaa ijayo.

Ukuta wa Taifa Stars ulikuwa imara sana hasa alipoingia Kibwana kukamilisha mapungufu ya mwanzo. Kibwana ambae alim "switch off" Victorien Adebayor ambae sasa alionekana ni kama mchezaji wa ndondo kapu na wakamtoa . Ukuta huu ukiongozwa na Mwamnyeto aka "Nesta" ni chuma cha pua ukifanana kama ule ukuta wa Italia chini ya Nesta na Maldini au Ujerumani chini ya Mathias Sammer!

Novatus Dismas aka "Modrić" ni hazina mpya ya Taifa Stars big up sana, kijana anaupiga mwingi mno pale katikati na ilipendeza sana alipocheza kwa dakika zote 90. huyu kijana akipumzishwa huwa tunapigwa magoli mengi sijui kwanini.

George Mpole si wa pole pole katika kucheka na nyavu. Hili ni tumaini jipya kwa Taifa Stars, kwa George nafasi moja tu umekwisha na alifanya kikamilifu alichotumwa Niger. Huyu ndie alietubeba Niger maana mpira ni magoli. Huyu ndie alietupa raha. Mpole ndie shujaa wetu kule Niger. Itapendeza sana kama Mpole akiweza kutupia goli mbili kila mechi atakayoanza badala ya goli moja. uwezo wa kufunga goli mbili kila mechi Mpole anao. Sasa iwapo Mpole atafunga magoli mawili, Samatta moja, Msuva moja, Kibu moja na Feisal moja ina maana kila mechi tuna uwezo wa kufunga goli 6. hii hesabu imekaa poa sana na inawezekana , hatutaki kosa kosa tunataka umakini uongezeke katika kulenga goli, tunataka magoli mengi, tunataka tuone nyavu za wapinzani wetu zitikisike. Uwezo huo wa kufunga Taifa Stars wanao maana tuna mechi nyingi tumecheza bila kupoteza.

Taifa Stars ilicheza vizuri sana vs Niger na timu imeimarika pakubwa mno hongereni sana vijana, dawa ni vijana kufanya mazoezi ya kukimbia muda mrefu na kuwa na pumzi ya kutosha kukaba na kushambulia kwa dakika tisini!maana ni kawaida ya hii timu kukata moto Dkk ya 60 na kuruhusu kushambuliwa hadi mwisho hatimae tunafungwa kizembe magoli kibao. Pia timu inapaswa kumchagua mtu wa kuanzisha mashambulizi na wenzake wamjue ili tuwin zaidi maana alikosekana mechi na Niger.

Sasa ni zamu yetu kwenda Afcon ambako wachezaji wetu wataonwa na timu kubwa na kupata soko ulaya. Kinachotakiwa ni kuwapiga Algeria ndani nje. Uwezo huo tunao kama wachezaji watajituma zaidi na Sureboy ataanza kikosi cha kwanza akiungana na kile kikosi cha baada ya Kibu kuingia.


nawasilisha
 
Mimi nilijua mmefunga goli limekataliwa, kwahiyo malalamiko FC mnataka muiendeshe mpaka timu ya taifa.
 
Refa alikuja na matokeo yake mfukoni ila ndiyo hivyo tena, hili suala TFF walifanyie kazi .
 
Kocha wetu amekariri majina ya wachezaji.

Mtu kama Msuva unampanga wa nini wakati huu hana timu, Msuva hana tofauti na mchezaji anayekaa benchi alafu unamwita timu ya Taifa alafu unamchezesha.
 
Refa alichezesha vizuri tu sema kocha alizingua kumtoa mchezaji mzalendo George Mpole na kumuingiza yule Mkongoman.

Zile nafasi alizozipata yule mkongoman angekuwa mzalendo George Mpole tungechukua point tatu bila kumlaumu mwamuzi.
 
Kocha wetu amekariri majina ya wachezaji.

Mtu kama Msuva unampanga wa nini wakati huu hana timu, Msuva hana tofauti na mchezaji anayekaa benchi alafu unamwita timu ya Taifa alafu unamchezesha.
Huna point. Kukaa benchi kwenye klabu uliopo haimaanishi huna kiwango kuliko wanaonza klabu nyingine. Vile vile kutokuwa na timu sio sababu ya kutoitwa timu ya taifa.
 
Refa alichezesha vizuri tu sema kocha alizingua kumtoa mchezaji mzalendo George Mpole na kumuingiza yule Mkongoman.Zile nafasi alizozipata yule mkongoman angekuwa mzalendo George Mpole tungechukua point tatu bila kumlaumu mwamuzi.
Utopolo kama utopolo
 
Kim ache kuita wachezaji wanaokaa benchi au wasioshiriki michuano yoyote leo tulimwona Msuva tofauti kiwango chake kimeshuka sana.
Wachezaji wamwachie nahodha kuongea na mwamuzi wajue haya ni mashindano ya kimataifa watapata kadi ambazo zitaigharimu timu
 
Kim ache kuita wachezaji wanaokaa benchi au wasioshiriki michuano yoyote leo tulimwona Msuva tofauti kiwango chake kimeshuka sana.
Wachezaji wamwachie nahodha kuongea na mwamuzi wajue haya ni mashindano ya kimataifa watapata kadi ambazo zitaigharimu timu
kwa mawazo yangu alikosekana Sureboy wa kumlisha mipira Msuva na George Mpole
 
Ila jamani mmemuona yule no.10 wa algeria...asije kutufanga kitu kibaya hapa taifa
 
Manula akiwa chini kalala kwa maumivu refarii aliuchukua mpira kutoka kwa kipa na kupuliza kipenga cha kumaliza mpira hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom