TFF kuanza kutoa odds za kubeti kwa kampuni za Betting

TFF kuanza kutoa odds za kubeti kwa kampuni za Betting

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
6,559
Reaction score
12,518
1747038768668.jpg

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwafahamisha wadau wa mpira wa miguu na umma kwa ujumla kuwa kuanzia msimu ujao wa 2025/2026 litakuwa na mshirika (partner) wa michezo ya kubashiri katika mashindano yake yote.

Mshirika huyo atashikilia haki hizo kwa kipindi chote cha makubaliano. Hivyo, yeyote mwenye nia au kuhitaji odds kwa ajili ya mechi ambazo zitakuwa chini ya TFF atalazimika kuwasiliana na mshirika huyo.

Makubaliano yetu na mshirika huyo yatakuwa ni kwa ajili ya odds tu, na si ushirika mwingine na kampuni za michezo ya kubashiri (betting companies) kama udhamini (sponsorship) au ushirikiano (partnership).

Utaratibu huu ndiyo unaotumika katika Ligi mbalimbali barani Ulaya.

Hatua hii ya TFF pamoja na mambo mengine, pia itazinufaisha kimapato klabu ambazo mechi zao zitakuwa zimeingia kwenye odds.

Licha ya malipo yatakayokuwa yanatokana na odds, bado klabu zitaendelea kudhaminiwa na kampuni hizo za michezo ya kubashiri, kwani utaratibu huu hauathiri makubaliano ya udhamini kati ya pande hizo.

Utaratibu wa kumpata mshirika huyo utafanyika kwa njia ya mnada utakaotangazwa wakati utakapowadia.
 
Ebu fafanua vizuri, sijakuelewa mkuu. Sasa wao TFF wanatoa hizo alama halafu wanampa nani? Wanauza au ni kama kivutio kwa mashabiki wa mpira?
Au inakuwaje?
Mhmmm shirikisho la mpira kutoa odds hii hata mimi sijui imekaaje master.
 
Hapa ndio utagundua kuwa mashabiki wengi hawaelewi nini kinazungumzwa hapa, wanajibu kwa mihemko tu...
 
Ni kama sijaelewa vile,yani tff ndiyo utakua unapanga odds mfano anacheza simba na yanga aseme yanga kushinda iwe odds 2.55 na simba kushinda iwe odds 3.55 nk
 
Iko hivi kampuni za kubet huwa zinatoa odds kwa kila timu kulingana na timu ipi inakutana na ipi. Lakini hizi odds huwa wanazinunua kwa wamiliki wa ligi husika... Hapa kwetu hiki kitu hakikuwepo ndio wataanza msimu ujao.
 
Iko hivi kampuni za kubet huwa zinatoa odds kwa kila timu kulingana na timu ipi inakutana na ipi. Lakini hizi odds huwa wanazinunua kwa wamiliki wa ligi husika... Hapa kwetu hiki kitu hakikuwepo ndio wataanza msimu ujao.
Kwa hiyo makampuni ya kubet itabdi yanunue mechi..!
 
Back
Top Bottom