TFF kuanza kutoa odds za kubeti kwa kampuni za Betting

Fala adriz sasa achana na mipira maana wana usika na kamari au unasemaje ?
 
Inamaana Tff itaingia mkataba na kampuni moja wapo ya kubeti, odds zote za mashindano ambayo yapo chini ya Tff zitakuwa chini ya hiyo kampuni. Hivyo kampuni zingine zote za kubet zitanunua odds kwa kampuni itakayoingia mkataba na Tff.
 
Inamaana Tff itaingia mkataba na kampuni moja wapo ya kubeti, odds zote za mashindano ambayo yapo chini ya Tff zitakuwa chini ya hiyo kampuni. Hivyo kampuni zingine zote za kubet zitanunua odds kwa kampuni itakayoingia mkataba na Tff.
Mimi nilidhani wangeondoa kabisa michezo ya kubashiri kwenye ligi yetu, hiki kinachofanyika ni kuwa wanabariki betting kwenye ligi yetu ambayo kwa sasa kuna tuhuma nyingi sana za rushwa na match fixing
 
Hatuchezi derby
 
Shida ni kwamba; hiyo TFF imejaa wahuni na vibaka. Halafu wanaingia mkataba na vibaka wenzao. Kitakacho tokea hapo, ni Mungu tu ndiyo anayejua.
 
Iko hivi kampuni za kubet huwa zinatoa odds kwa kila timu kulingana na timu ipi inakutana na ipi. Lakini hizi odds huwa wanazinunua kwa wamiliki wa ligi husika... Hapa kwetu hiki kitu hakikuwepo ndio wataanza msimu ujao.
Kwahyo hii inaweza saidia kuwepo kwa michezo yetu kwenye websites za betting hata kabla ya siku kadhaa za mchezo kufika,tofaut na sasa ambako michezo inapatikana siku ya mechi
 
Ebu fafanua vizuri, sijakuelewa mkuu. Sasa wao TFF wanatoa hizo alama halafu wanampa nani? Wanauza au ni kama kivutio kwa mashabiki wa mpira?
Au inakuwaje?
Swali zuri sana.

Katika ligi ya Tanzania (na ligi nyingine za kiwango cha kati au cha chini), bookmakers wanakompaseti odds kwa kutumia vyanzo vifuatavyo:

1. Data kutoka makampuni ya takwimu (sports data companies)
Makampuni kama Sportradar, Stats Perform, au BetRadar hukusanya data za mechi — matokeo, wastani wa magoli, kadi, majeruhi, n.k. Hii data ndiyo msingi wa kutengeneza odds hata kwa ligi kama ya Tanzania.
Sasa hapa ina maana akina Karia wataingia mkataba na hiyo kampuni kisha kampuni zote za kubeti zitanunua odds kutokea huko na wao wanapata faida.
2. Algorithm ya odds
Bookmakers hawakai tu kuangalia Simba na Yanga kwa jicho la kawaida — wanatumia algorithms (models) zinazopima:
  • Mechi za nyuma
  • Ufanisi wa nyumbani vs ugenini
  • Form ya wachezaji
  • Uwezekano wa sare
  • Lineups zinazotarajiwa
  • Motivation (mf. Simba ikishinda inapata ubingwa — motivation kubwa)

3. Market movement (betting market)
Kama watu wengi sana wanaweka hela kwa timu fulani, odds zake huanza kushuka ili kudhibiti hatari ya kampuni kupata hasara. Mfano:
  • Odds za Simba zilianza 1.90 tuseme dhidi ya Nyuma mwiko
  • Lakini watu wengi wakaweka hela kwa Simba
  • Odds zinashuka kuwa 1.60 au chini zaidi ili wasipate hasara kubwa kama Simba atashinda kweli

4. Experts wa ndani (local scouts)
Bookmakers wakubwa wanaajiri watu wa ndani wanaofuatilia ligi ya Tanzania, wanapeleka ripoti kama kuna mabadiliko muhimu (mfano mchezaji muhimu kaumia, au kuna matatizo ya kiutawala ndani ya timu).

KWA MSAADA WA NTANDAO
 
Hio Haiwezekaniki hata siku moja wewe kama mdau unaweza ukatoa ODDs vyovyote unavyotaka ingawa ODDS zako zikiwa tofauti unatengeza arbitrage hivyo kuweza kupoteza; kupata hizo odds ndio maana unakuta odds huwa zinafanana na hazina tofauti kubwa..., TFF kama TFF ina ujuzi gani wa kuweza kufanya hivyo au unaweza vipi kuwapangia wadau

Nina wasiwasi na huu ujumbe kama ni authentic au unachodhani sio walichomaanisha
 
Iko hivi kampuni za kubet huwa zinatoa odds kwa kila timu kulingana na timu ipi inakutana na ipi. Lakini hizi odds huwa wanazinunua kwa wamiliki wa ligi husika... Hapa kwetu hiki kitu hakikuwepo ndio wataanza msimu ujao.
Hakuna kitu kama hicho eti odds wanazinunua kwa wamiliki wa ligi husika .
Nimejaribu kufatilia sana sijaona hicho kitu
Embu leta uthibitisho kwamba odds zinanunuliwa kwa wamiliki wa ligi.

Acha uongo tff ni wahuni tu wanataka kutengeneza change cha mapato.
Kwa mpira wetu wa bongo kampuni nyingi za betting hazitanunua hizo odd na .
Odds zinatengenezwa na makampuni ya kubett yenyewe ndio maana unaweza kuta mechi ya liverpool vs arsenal inakuwa na odds tofauti tofauti katika matokeo sawa kwenye makampuni tofauti.
Sio kweli kwamba odds zinatengenezwa na wamiliki wa ligi na wanaziuza
 
Ni kama sijaelewa vile,yani tff ndiyo utakua unapanga odds mfano anacheza simba na yanga aseme yanga kushinda iwe odds 2.55 na simba kushinda iwe odds 3.55 nk
Ndio manake ila kiuhalisia sio kweli kwamba wasimamizi wa ligi ndio wanatengeneza odds na kuziuza kwa kampuni za betting hakuna kitu kama hicho dunia nzima .
 
Watuletee odd kama za SERIA A maana zmekaa vzur kama zle za fiorentina siku ya leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…