kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Haji Manara ameshiriki kuuwekea taswira mpya mpira wetu Tanzania. Hamasa ya mpira tanzania imekuwa kubwa sana katika kipindi cha Haji. Haji amesababisha watu sasa wanakwenda wengi viwanjani kuangalia football jambo ambalo watu wanafahamu hivyo, serikali inajua, bunge linafahamu, TFF inajua, CECAFA wanafahamu na hata CAF inafahamu mchango wa Haji kwenye football ya Tanzania.
Watu wakijaa uwanjani mapato kwa TFF na wadau wengine yanapanda pia, kumfungia haji ni kupunguza hamasa ya mpira nchini na kujikosesha mapato pia, yaani kujipiga wenyewe risasi ya mguu. Ni kama EU walivyoiwekea vikwazo Russia ambavyo vinawarudia wenyewe. Afrika wanaitambua Tanzania sasa hivi kutokana na hamasa ya mashabiki wetu kuupenda mpira ndani na nje ya uwanja. Haji sio kama watu wengine, tumsamehe tu hata kama hatupendi ila kwa maslahi ya mpira wetu.