sixgates
JF-Expert Member
- Mar 19, 2011
- 3,979
- 1,665
Kila siku tumekuwa tunajiuliza kwanini watanzania wengi wanafuatilia ligi ya uingereza kuliko ligi yoyote duniani. Jibu ni moja tuu..inatangazwa sana..lakini sio utangazaji kama tunavyotangaziwa vifurushi vya tigo ama voda..bali ni branding kwa wachezaji. Ligi kuu tanzania bara imezidiwa ujanja na NDONDO CUP kwani toka mwezi uliopita vibanda vingi vinaonyesha mpira wa miguu ndondo.. lakini siku ya leo kila mtu hapa mjini alikuwa akizungumzia Kauzu fc na aina yao ya ushangiliaji, mbwembwe na kila kitu. Nlichojifunza leo kauzu fc vs temeke market.. wanaotangaza hiyo ligi wameachana na kuonyesha mpira ila wameamua kuonyesha ushangiliaji dhidi ya hivi vikundi viwili. Na bado hiyo ni nusu finally bado hawajacheza finally..TFF wasipokuwa smart people will eventually believe ligi kubwa tanzania ni Ndondo cup inayosimamiwa na clouds. Toka michuano ianze wanahudhuria wasanii, wafanyabiashara, wanawake, mawaziri na leo hii nimemuona mkuu wa mkoa wa Dsm.