TFF Kuna tatizo gani?

Malinzi ni shida tangu alipoingia TFF..... kwanza alienda kupanga ofisi PPF Tower kwa kuona kukaa ofisi za Karume ataonekana kama yeye siyo CEO ni lazima akakae na MA_ CEO wenzake posta. Pili akafanya ubadhirifu wa kutisha kwa kizingizio cha kutafuta vipaji nchi nzima... matokeo yake zoezi zima halikuwa na tangible results. Ameshidwa kuongoza TFF kwa maana hili suala la kodi alitakiwa amelishughulikia na serikali na kulimaliza. Yeye amekuwa mtu wa kulalamika sana
 
Huyu jamaa chuakachara naona hoja zake ni kumtetea malinzi hivi kuna kaundugu nn? Au mwenzetu unasehemu ya posho pale au ni wa kabila lako ndugu maana huna hoja bali kubwabwaja tu wewe huoni mpira unakoenda,umeomba solution ok moja jamaaa yako ajiuzuru mengine nitakuambia baada ya kufanya hivyo
 
Bado hujatoa hoja /solution. Atoke aingie ndugu yako. Toa justification, a scientific one kwa nini atoke na atakayekuja atafanya nini na matatizo yaliyopo. Eg, Mkwasa ishu ya mshahara wake aliiacha aliyetoka. PAYE ya makocha wa kigeni ni utawala uliotoka etc Madeni ni toka kipindi hajaingia madarakani. Usimlaumu mtu kabla ya kufanya research kuona undani wa tatizo
 
Kama hoja ni kuingia nani mbona mlilalamika juu ya raisi kikwete na alipotoka ameingia magufuli amefanya mabadiliko au hajafanya? Kama hoja ni madeni ya nyuma hata srrikali yako ina madeni ya nyuma lkn mfano magufuli anaonesha njia za kupambana nazo nchi iwe salama sasa kama huyo kaka yako aliyakuta amefanya nn kutatua? Mbona hutumii akili ndogo sana hata kufikiri hivi kosa likiwa ni la nyuma kwa hiyo wewe kazi yako kukaa tu huna hata strategies za kufumbua,
Wewe jamaa una lako jambo na huyo
 
Hii tff hakuna kitu yaani tutamkumbuka Tenga heri angetua Wambura
 
Lakini namsifu Malinzi kwa ujasiri wake usio wa kawaida wa kuhamishia ofisi za TFF kutoka Uwanja wa Karume hadi kwenye ghorofa la kifahari down town kwa pango kubwa, huku wakijinadi kuwa hawana pesa za kutosha kuendeshea na kusimamia soka! FIFA na wenye akili waliwashangaa!!
 
Aisee hata mimi hapo nilicheka kwa uchungu
 
Then give him time to make the needful. Magufuli has financial power, your example does not compare well with that of TFF dealings.
 
Jamani eeh mnyonge mnyongeni haki yake mpeni si tu Malinzi, hakujawahi kuwa na uongozi mzuri TFF, si kwa Ndolanga wala Tenga. Hakuna maendeleo kama tafsiri halisi ilivyo. Tunaofahamu mpira na trend ya soka letu..hakuna wa kumpa A. Bado hatuna cha kujivunia ktk soka. Nchi haina falsafa ya soka unategemea nini?
 
Upo sahihi kabisa TFF pale hamna kitu,miaka yote ni magumashi tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…