Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 384
- 970
TFF hebu oneni aibu basi, inakuwaje Tuzo za ligi ya msimu huu zikafanyike mwanzo wa msimu mwingine?
Hili linashangaza sana maana mmeamua kuvunja hata kanuni yenu wenyewe kwa sababu Kanuni ya 11 inayozungumzia Vikombe na Tuzo, kifungu cha (11) kinasema; Sherehe za tuzo zitafanyika ndani ya muda usiozidi siku tatu (3) baada ya kumalizika kwa mchezo wa mwisho wa Kombe la Shirikisho.
Maana yake mara tu baada ya mechi ya fainali ya FA Zanzibar, zilitakiwa zisizidi siku tatu sherehe za tuzo zifanyike, sasa nyie mmeamua tu kuivunja kanuni hiyo ili kuvuruga mambo kwa kuwa tuzo zitakapofanyika wakati wa Ngao ya Jamii msimu ujao, kuna wachezaji watakuwa wamepewa 'Thank you, wengine hawatakuwepo kabisa hapa nchini na wengine mfano wanaweza kutajwa fulani ni kipa bora kutoka Azam FC kumbe wakati huo labda atakuwa amehamia Simba. Sasa mtamtaja kama kipa bora kutoka Azam au Simba?
Haipendezi, haipendezi kabisaaa.
Mlianza kufanya mambo kivyenu vyenu kwa kuanzisha Ngao ya Jamii ya timu nne, jambo ambalo halipo popote ulimwenguni, tukawasamehe.
Mkaleta siasa za kuhamishia fainali ya michuano ya FA ya Tanzania Bara, visiwani Zanzibar ambako ni kama nchi nyingine kwa kuwa na wao ni wanachama wa CAF na wana mashindano yao ya ligi na FA pia, tukawakaushia pia, sasa na hili la tuzo, hapana.