TFF kwa hili Wingu, Mvua hii Kubwa na Hali ya Hewa isiyo Rafiki msione Aibu tu Kuahirisha Derby ya Leo kwa Mkapa

TFF kwa hili Wingu, Mvua hii Kubwa na Hali ya Hewa isiyo Rafiki msione Aibu tu Kuahirisha Derby ya Leo kwa Mkapa

Mpira utaahirishwa "ikilazimu", timu zikiwa uwanjani. Wakiahirisha kwa kukurupuka, hawaachi kugeukana.
 
Sasa Ni Saa 5 inaenda Saa 6 Mchana na Hali ya Hewa ni ya Mvua, Baridi na Upepo tusidanganyane kuwa Hali ya Hewa hadi Saa 11 Jioni muda wa Mtanange ( Mechi ) hii Mvua itakuwa imekata.

TFF na TPLB nawashauri I msione Aibu au kuingiwa na Uwoga kutangaza muda huu ( mapema hii ) kuwa Mechi ya Simba na Yanga imehairishwa kutokana na Hali ya Hewa mbaya ya Mvua Kubwa zinyeshazo sasa na kwamba ichezwe Jumatano ijayo au ipangiwe tarehe nyingine / mpya ila kwa GENTAMYCINE sioni dalili zozote za kuwepo kwa Mechi ya Leo na Mpira ukawa ni wa Kuvutia na Watu ( Mashabiki ) Kuufurahia.
Kwa wenzetu wangeshatuma watathmini na Mechi ingetangazwa PP Tangu saa 6, huku Ughaibuni mpaka maji yawe yanafika kiunoni kwa mchezaji ndo Mechi iahirishwe.
 
Ni vyema maboresho mapya ya uwanja yaendane na kuwa na kifuniko au turubai maalumu kwa juu la kufunga na kufungua ili nyakati kama hizi mambo yasiharibike....
Hili wazo sijawahi kulifikiria Ila ni bonge la idea. Hata Hilo turubai lingewekwa kwenye pitch Tangu Jana Mambo yasingeharibika.
 
Kwa wenzetu wangeshatuma watathmini na Mechi ingetangazwa PP Tangu saa 6, huku Ughaibuni mpaka maji yawe yanafika kiunoni kwa mchezaji ndo Mechi iahirishwe.
Huko huko kwa wenzenu kila siku watu wanacheza mech kwenye barafu, sio tu mvua,

Acheni kuwadekeza watu, hakuna mvua kubwa ya kuzuia match hapa, hii match ichezwe,
Ingekuwa kagera sugar Vs Mtibwa mngekuja kulalamika ?
 
Kweli Kagera Sugar Vs Mtibwa Sugar ni Sawa na Simba Vs Yanga Mkuu? Si Sawa kulinganisha Hiace na Macopolo.
 
Kweli Kagera Sugar Vs Mtibwa Sugar ni Sawa na Simba Vs Yanga Mkuu? Si Sawa kulinganisha Hiace na Macopolo.
Utofaut wake nini? Si zote zinacheza NBC ? Kwa akili hii ndio mana unataka hii iahirishwe ila nyingine zichezwe kwenye mvua 😂😂😂😂 sasa kwa taarifa yako goma linapigwa kama kawaaa
 
Back
Top Bottom