TFF: Kwa waamuzi wa aina hii msitegemee maendeleo ya soka

TFF: Kwa waamuzi wa aina hii msitegemee maendeleo ya soka

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Niko uwanja wa Kambarage Shinyanga naangalia mechi kati ya Stand United na Mtibwa. Kuna tukio limetokea kwenye mechi hii dakika ya 7 labda niliweke hapa wajuzi Wa sheria za mpira mlijadili. Mchezaji Wa Mtibwa kafanya faulo mita kama kumi kutoka kwenye box la 18 la upande wake. Refa akapuliza filimbi na kuhesabu hatua 10 toka kwenye mpira na kuwaamuru wachezaji Wa Mtibwa waweke ukuta. Wao wakahesabu hatua 8 wakaweka ukuta wao tofauti na alipowaelekeza Refa. Hata walipoelekezwa waligoma na ukatokea ubishi kati yao na Refa kama dk 4 nzima. Ili kumaliza ubishi Refa akawaacha walipoweka ukuta akarudisha mpira nyuma hatua 2 na faulo ikapigwa. Je, kwa waamuzi kama hawa wanaogomewa na wachezaji na wao kulazimika kufuata maamuzi ya wachezaji tutegemee nini mechi ya ligi kuu inachezeshwa kama chandimu?
 
Huyo refs dhaifu tu yeye mwenyewe!!!
 
Huku taifa washabiki ndio wanamuongoza muamuzi kutoa kadi
 
Huku taifa washabiki ndio wanamuongoza muamuzi kutoa kadi
Hivi ukifikiri kwa umakini na utulivu unadhani ile aliocheza Mao Bufu haikustahili kuwa Kadi nyekundu?! Usijitoe ufahamu mkuu kisa ushabiki wa Simba na Yanga.! Football is a game of fair play
 
"Football is a game of fair play" ulitaka atoe kadi kw timu zmima ama? Au wangeendelea kubishana mpaka mda huu?Alivyofanya ni sawa na hio ndo fair play
 
Back
Top Bottom