TFF mchezaji wa 13 Simba?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kati ya TFF na wanachama wa Yanga ni nani mwenye timu? ni nani mwenye uchungu na timu?

Yanga kwa sasa ina shida ya pesa na mdhamini lakini sio Mwenyekiti wala viongozi. Timu ya Yanga kipaumbele chake kwasasa sio uchaguzi bali pesa.

TFF iisaidie Yanga namna ya kupata pesa na mdhamini mwenye hela kama mo ili kuwalipa wachezaji wa Yanga.

Timu ya Yanga iko vizuri uwanjani hawahitaji uchaguzi utakaosababisha yanga kufanya vibaya na kutoa nafasi kwa Simba na Azam (ni ndugu hawa) kitendo ambacho kitatafsiriwa na wadau wa Yanga kama mkakati wa kuidhoofisha Yanga uwanjani ili kuzipatia nafuu Simba na Azam kwenye ligi.

Itaonekana kama vile TFF inawaongezea nguvu wachezaji na mashabiki wa Simba na Azam uwanjani ili wapate matokeo.

Yanga waachwe wenyewe watafute njia na wakati mwafaka wa kufanya uchaguzi wao, maana kama ukiitisha mkutano mkuu leo wa wanachama wa Yanga uchaguzi wa Januari hautakuwa kipaumbele chao kwasaababu hawaoni uhusiano wa moja kwa moja kati uchaguzi huo na kupata pesa za kuendesha club yao.
 
Mambo ya ngoswe yaachiwe ngoswe wenyewe waamue. TFF waisaidie yanga kumlipa Kakolanya arudi kikosini akaidakie club ili iendelee kufanya vizuri kwenye ligi na sio kuisaidia kufanya uchaguzi unaosababisha vurugu kwenye club
Well said Mkuu,watuachie Yanga Yetu
 
 
Kikubwa sheria ifuatwe.
Timu inataka Mwenyekiti au matokeo uwanjani? Mwenyekiti yupo na kila mtu anafahamu shida zilizompata ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake kama binadamu. Hivyo wanachama wa klab ya Yanga walimuelewa na wakakubali kumvumilia wakati anaendelea kutafakari kilichomtokea na kukarabati afya yake. TFF hamhusiki kabisa na hilo maana hakuna aliyewalalamikia. Ni heri muitishe mkutano wa wanachama ili msikilize maoni yao kuliko kulazimisha kupandikiza mgogoro yanga katikati ya ligi. Ndiyo maana tunajiwa na mawazo ya usimba na uyanga hapa. Watu wanafikiri kuwa huenda hali ingekuwa tofauti kama Yanga ingekuwa inaburuza mkia kwenye ligi inayoendelea.
 
Mkuu hii post yote ya nini? Ushabiki usikutie upofu kwenye mambo ya msingi. Mimi pia ni shabiki wa Yanga ninayependa pia soka la nchi hii lifike mbali. Hili saga linaloendelea kati ya TFF na Yanga sijalifuatilia na ndo mana sijatia neno zaidi ya kusema sheria ifuatwe.

Kama TFF wana mamlaka hayo kisheria wafanye wanavyoona inafaa haijalishi timu itaathirika au vipi ila kama hawana Yanga wanajua cha kufanya.

Tumefika hapo tulipo kwaababu ya kupindapinda mambo.

Narudia tena KIKUBWA SHERIA IFUATWE.
 
Reactions: Tui
Kwani simba walipokua wanafanya uchaguzi ilikua ni kuipa nafasi yanga?
 
Timu kuwa na viongozi ni wajibu na haki. Kama tukiendelea na hii tabia basi ipo siku timu haitafanya uchaguzi miaka mia, chama cha soka hwatafanya uchaguzi eti hatuhitaji uchaguzi, au ipo siku watakatalia madarakani kisa hawataki uchaguzi
 
Sheria ipi? Kama ni kuvunja sheria basi kutowalipa wachezaji stahiki zao ni uvunjifu wa sheria mkubwa kuliko hata kujazia mapengo ya viongozi waliojiuzulu kwa sababu za msingi.

Heri tff iwasaidie ushauri wa namna ya kuwalipa wachezaji wanaodai hela zao kwanza
 
Timu kuwa na viongozi ni wajibu na haki. Kama tukiendelea na hii tabia basi ipo siku timu haitafanya uchaguzi miaka mia, chama cha soka hwatafanya uchaguzi eti hatuhitaji uchaguzi, au ipo siku watakatalia madarakani kisa hawataki uchaguzi
Hiyo ni kazi ya wanachama wenyewe, tff isubiri kupelekewa malalamiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…