Aaaa! Beno nae hasomi alama za nyakati, kazi yake ya ugolikipa ni kazi takatifu haitaki vitendo kama hivyo alivyofanya.
Hakuna timu makini duniani itapenda golikipa mwenye historia ya tabia kama hiyo ya kugoma anapokuwa na shida hasa ya kifedha. Hii ina maana kuwa golikipa kama Beno ana uwezo wa kuchukua fedha kutoka timu pinzani na kuiuza mechi.
Aliyemshauri Beno kufanya hivyo alikosea sana kupita kiasi. Beno hataaminika pahala popote duniani kucheza kama golikipa, maana hawatajua akikasirishwa na uongozi atachukuwa hatua gani kama sehemu suluhisho ya shida yake.