Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,753
- 10,747
[http://phpstack-189796-562565]
Huko TFF hata mipira ya kuchezea ligi kuu hakuna
Today, 2h ago | Shabiki NambaMoja
Inaelezwa timu za ligi kuu zimekuwa zikitumia mipira yao katika michezo inayochezwa kwenye viwanja vya nyumbani kutokana na 'ukata' unaoliandama Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
Siri hiyo imefichuka juzi baada ya kukosekana mipira ya kuwapa wachezaji wawili wa Simba Meddie Kagere na Emmanuel Okwi waliofunga mabao matatu kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union
Ilibainika Simba ilitumia mipira yake kwenye mchezo huo na mipira waliyopewa wachezaji hao ilienda kuchukuliwa stoo ya TFF
Mwenyekiti wa Bodi ya ligi Steven Mguto amekiri kuwepo kwa uhaba wa mipira hali iliyokithiri baada ya ligi hiyo kukosa mdhamini
"Ni kweli msimu huu wamekuwa tatizo na uhaba wa mipira kwenye mechi zote za Ligi Kuu Bara na si Simba ambao wanatumia mipira yao, bali hata timu nyingine wanapokuwa wanacheza mechi zao huwa wanatumia mipira yao," Mguto amenukuliwa na Mwanaspoti
Aidha Mguto aliongeza kuwa mipira ya kutoa zawadi kama mchezaji akifunga mabao matatu katika mchezo mmoja (hat trick), ipo lakini ile ya kuchezea katika hali ya ushindani ndio tatizo msimu huu baada ya kukosa wadhamini wa ligi
"Juhudi kubwa za kumtafuta mdhamini kwa upande wetu zinafanyika lakini miongoni mwa makubaliano ambayo tutaingia nae ni kutupatia mipira iliyokuwa bora na tutaigawa katika kila kituo ili kuweza kutumika katika mechi za ligi na kuondoa kabisa uhaba ambao tumekutana nao msimu huu"
Hakika kama hakutakuwa na mabadiliko makubwa ya kimfumo katika uendeshaji wa soka la Tanzania, itakuwa ndoto kwa timu zetu kufikia mafanikio makubwa katika ngazi ya Kimataifa
My take.
Nyie ni taasisi kubwa sana haiwezekani na haingii akilini kabisa kitendo kama hiki kitokee.
Kama kweli mnaweza kushindwa kuwa na mipira jambo ambalo sidhani kama linahitaji wadhamini je kweli mnaweza kusimamia ligi vema?
Hii ni aibu sana.