TFF mkiwa ' Watiifu ' hivi kwangu kwa kufuata kile ambacho huwa nawaambia basi mtakuwa Marafiki zangu na nitawapa Ushirikiano

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ni mwishoni mwa Wiki iliyopita tu GENTAMYCINE nilianzisha Uzi hapa wa ' Kukasirishwa ' na Kitendo cha Kocha wa Taifa Stars pamoja na TFF yake Kutomjumuisha Kikosini Kipa ' mahiri ' na Tanzania One Kwangu kwa sasa Golikipa wa Simba SC Aishi Salum Manula kwa sababu zao za ' Chuki ' Kwake na nikaonya kuwa kwa ' Ushahidi ' nilionao ya kwanini Manula alikuwa haitwi Kikosini kama asingeitwa katika Uteuzi wowote ule ujao basi ningeenda ' Kuwaanika ' Wahusika wote ili ' Waumbuke ' na Watanzania wawajue.

Nashukuru ya kwamba leo Kocha Mkuu wa Taifa Stars amemuita Kikosini Kipa Aishi Salum Manula kama ambavyo nilitaka hivyo nami GENTAMYCINE nasema rasmi kuwa sitoenda ' Kuwaumbua ' hao Wahusika Wakuu toka TFF ambao ndiyo walikuwa wakisababisha Aishi Manula asiitwe Taifa Stars. Nilikuwa nikishangaa na Kujiuliza mno ni kwanini Kipa Aishi Salum Manula ambaye yupo katika Kiwango chake bora kabisa kwa sasa kila Kocha akifanya Uteuzi wake alikuwa hamjumuishi / hamuiti Kikosini.

This is GENTAMYCINE.
 
Kuitwa na kucheza ni vitu viwili tofauti,ataendelea kukalia mkeka.

Kikubwa nilichokitaka na Lengo langu Kuu la Kocha wa Taifa Stars kupitia TFF wafanye kila wawezalo Kipa bora Aishi Salum Manula aitwe Kikosini limetimia na najiona Mshindi. Kuhusu Kupangwa au Kutopangwa hayo ni Maamuzi ya Kocha japo ' Kiufundi ' kwa sasa Kipa Manula anatakiwa Kuanza kwani kwa Siku za Karibuni Kipa Juma Kaseja ameshuka Kiwango na hana Kubwa zaidi ya Kujivunia Kudaka Kwake tu Penati kitu ambacho hata Kipa Manula anakiweza vile vile. Pamoja na Uzuri ( Umahiri ) wake Kipa Juma Kaseja huku wengi Wenu mkimsifu ila Penati za Juzi kati kutoka kwa ' Mafundi ' Walibya hakuziona na alifungwa Goli la Kipuuzi kabisa ambalo hata Kipa wangu wa MabangiGongo FC asingefungwa.
 
....hata sijawahi kuuona huo ubora wa Manula, sijaona hiyo title ya tz one kama anaistahili, kipa muoga asieweza linda eneo lake inavyostahili, hajiamini, sikuona sababu ya simba kufungwa zile goli 5 misri manula aliwa golini., yani hata muarabu akipiga mpira vibaya bora uelekee golini tu, tunafungwa! ,bora Kakolanya nae apewe nafasi nimuone..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…