kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kitayosa timu ngeni kwenye ligi yenye wachezaji 8 TU bila benchi la ufundi Wala mchezaji wa akina ililazimishwa kucheza na Azam kamili kwenye mchezo wa ligi kuu. Lakini Simba iliyokuwa na wachezaji 3 TU muhimu wenye mafua TFF na bodi ya ligi waliwakubalia kuahirisha mechi Yao kule Kagera na kuisogeza mbele. Kulikuwa na ugumu gani TFF na bodi ya ligi kuisogeza mechi mbele kidogo?
TFF hivi mna nini lakini?
Vitendo hivi mbali ya kuwa double standard lakini inazalisha washindi wa ligi legelege na mfungaji Bora bandia.
====
Mchezo wa Azam FC dhidi ya Kitayosce FC ya Tabora umemalizika kwa Azam FC kupata ushindi wa magoli 4-0, huku mchezo huo ukivunjika dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza.
Kitayosce waliokuwa Wageni wa Azam FC katika uwanja wa Azam Complex, walianza mchezo huo kwa kuwa Wachezaji wanane uwanjani huku Azam FC wakiwa 11.
Wakati mchezo unaendelea golikipa wa Kitayosce na Mchezaji mmoja wa ndani aliumia hivyo mchezo ukashindwa kuendelea dakika ya 27 kutokana na kubaki 6 uwanjani na kanuni zinaruhusu mechi kuendelea endapo timu moja itakuwa na wachezaji kuanzia saba.
Hivyo kutokana na mchezo huo kuvunjika Azam FC anapata ushindi wa point 3 na magoli manne (Feitoto 3’ 9’ 13’ Dube 5’).