TFF MMEIHUJUMU SIMBA SC

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
Itoshe kusema kitendo cha kuwasimamisha waaamuzi waliochezesha Mechi ya TPL kati ya SIMBA SC na KMC ambao ni Bw.Kambuzi na wasaidizi wake kimekuwa Kaburi/Hujuma/Hitimisho la mechi za Simba SC kuchezeshwa kwa sheria 17 za soka.
Waaamuzi wanachezesha mechi za Simba kwa woga huku wakiiiminya Simba kuogopa rungu la TFF. Nasema kitendo hiki kilichofanywa na TFF ambacho mimi nakiita uhujumu wa mechi za Simba, kimeanza kuzaa matunda ambayo TFF walitaka. Wachezaji wa Simba wameanza kuuumizwa Maksudi na Waaamuzi hawachukui hatua stahiki, Simba inanyimwa FAULO za wazi nyote mnajua ingawa mmekaa kimia.
Tujiulize TFF ilikusudia nini kuchukua maamuzi yale kwa Kambuzi bila kusubiri kamati ya saa 72.
JE, MWAMWUZI wa Azam vs YANGA aliyekataa Goli la Donald Ngoma na kuchezesha mechi nzima bila kufuata sheria 17 mbona hajachukuliwa hatua mpaka sasa?
Je kilichotokea jana kule Mbeya kwa uchezaji usio wa Kiungwana Mbeya City dhidi ya Simba mmechukua hatua gani.
Mpango wenu huu nyie TFF hautafanikiwa kwa Simba hii iliyojaa Wachezaji, Viongozi na Wananchama wenye akili kuliko nyie. Mlikosoma hiyo mbinu chafu sisi ndio walimu. Mchezo mzima unafahamika mpaka waliotekeleza hivyo jihadharini sana na Simba SC itawapeleka walipo akina Malinzi et Al.
SIMBA NGUVU MOJA DAIMA.
 
Upuuzi wa soka la Tanzania. Huyu ukute ni kiongozi katika timu!!!
 

Nitakuja kulijibia hili Saa 4 Kamili za Usiku wa leo pale niki ' Log In ' tena hapa.
 
Simba wote wanawake angalieni tupu zenu. . Wanaume walivyokuwa wakigonbania Uhuru nyie mkaungana na wakoloni. . Wanawake tu bisha
 
Simba wote wanawake angalieni tupu zenu. . Wanaume walivyokuwa wakigonbania Uhuru nyie mkaungana na wakoloni. . Wanawake tu bisha
Though am not a fan of the said club, this is 'Irrelevant' answer basing to the issue being discussed.
 
Ni ukweli usio pingika Simba inabebwa na mabwana Karia Bonny wambura na katibu mkuu wa kuchonga kwa mbeleko ya chuma
 

Siko hapa Kuisema TFF au Simba SC ila ninachokijua tu ni kwamba mateso haya ya Uchovu ( Fatigue ) kwa Wachezaji wetu wa Simba SC tumeyataka wenyewe kwani tulikuwa bado tuna uwezo wa Kipindi kile kile tunashiriki ' Champions League ) kuwaambia TFF tucheze Mechi zetu ila Kiburi chetu Simba SC kilikuwa juu na sasa ni kweli tunashinda japo kwa taabu lakini Kiufundi tunawatesa mno Wachezaji wetu ila tuwashukuru tu kuwa na Wao ( Wachezaji ) wanapambana na kujituma Uwanjani ili tu kutupa raha wana Simba SC ili tuutetee Ubingwa wetu kwakuwa tayari wameshaona Utamu wa hiyo Michuano.

Tatizo la TFF liko sehemu ndogo sana nayo ni kwamba haipo imara ( Firm ) yenyewe kama Taasisi kiasi kwamba inaziogopa mno hizi Timu mbili Kongwe na siyo Kubwa barani Afrika za Simba na Yanga. Wakibadilika katika hili basi Soka la Tanzania litakuwa haraka na mafanikio kutokea. TFF haionei Simba SC au Kuipendelea Yanga SC isipokuwa tukumbuke kuwa Waamuzi ( Referees ) nao ni Binadamu na mara nyingi Mechi za hizi Timu Kubwa za Tanzania huwa na ' Pressure ' kubwa kiasi kwamba unaweza Kukuta Mwamuzi mahiri na makini akaharibu mchezo na sababu kubwa ikiwa ni Kitete kama siyo Kihoro.

Mwisho nikuhakikishie tu ya kwamba ni kweli Mechi za Simba SC zimepangwa mfululizo na Wachezaji wetu wana hiyo ' Fatigue ' ila Timu zote ambazo zitacheza na Simba SC katika Mechi zake Kenda / Tisa zilizobaki hata zije na Kukamia vipi au na ' Plan B ' zipi bado uwezo Wao wa kuweza Kucheza na Simba SC na kuizuia ndani ya dakika zote 90 ni ngumu na zote zitapokea Kichapo na hatimaye mwishoni Simba SC tutatetea tena Ubingwa wetu na amini kuwa Simba SC inaenda kuwa Bingwa tena Msimu huu kwa mara ya pili mfululizo.

Yangu ni haya tu ambayo nilikuahidi pale Jioni kuwa nikija tena hapa Jamvini ( JamiiForums ) Saa 4 Kamili hii ningekujibu.
 
Tff haiwezi hujumu mbelekl fc maana ni timu yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…