@Tff Mnajua kuwa wachezaji wengi wametoka kupitia mifumo isiyo rasmi ya Soka?

@Tff Mnajua kuwa wachezaji wengi wametoka kupitia mifumo isiyo rasmi ya Soka?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Kauli ya Raisi wa Tff leo ukitaka kuandaa Ndondo cup lazima upitie na upate kibali kutoka kwao.kwa hili hata siku zijazo Somalia watakua juu yetu kisoka kwenye rank za Fifa.

Wameona bwana flani anafaidi sana nini?vijana tukimbilie wapi tena hata kwenye Ndondo cup mnatuwekea kauzibe!tungezijua wap kauzu fc,abajalo fc?mkitaka nanyi mashindano yenu yapendwe basi mjitaidi kuyaboresha na sio kuanza kuwawekea wadau wengine wa soka giza.

Muulize Suarez yule wa Barcelona aliyefunga goli la kwanza dhidi ya madrid la pili likifungwa na Messi na msumari wa Tatu ukigongwa na Vidal.Suarez hajawahi kucheza michezo yoyote inayotambuliwa na chama cha soka cha nchi yake katoka kupitia Street football ila leo ni hatari nyingine.

Muulize Gabriel Jesus kacheza Ndondo cup mara ngapi karibu na ufukwe wa Copacabana kule Brazil je chama cha soka cha Brazil kinazijua hizo ndondo cup?vipaji vya mpira vipo ngazi za chini ambazo hata hazitambulika na nyie Tff.

Tengenezeni sera madhubuti ya kukuza mpira wetu na sio kuanza kupiga kelele na ndondo cup.
 
TFF wasitafute mchawi.Wao wanaandaa ligi zisizo na ubora wala msisimko wanakuja kulia na watu wanaoamua kuwa wabunifu na kuandaa mashindano yenye mvuto,wao wakomae na was wawe wabunifu kwenye mashindano yao.
 
wapuuzi tu sasa huku mikoani burudani yetu ndio izi ndondo cup hasa vijijini leo wanataka vibali wajinga sana.
 
Ukiwa shabiki wa Barcelona raha sana...unayakumbuka magoli yote mliyofunga![emoji16]
 
Verygood .....TFF.
Next step...... TFF taifisha vilabu vyenye mapato makubwa.
Baadae.......TFF wawe waendeshaji wa mashindano ya soka ya mashule na mashirika ya serikali na umma.
Halafu.......timu ya bunge ipangiwe ratiba.
 
Rais wa mpira tumempata kwa kweli.........
Mpaka mwakani Tanzania Mwezi kama huu Tutakuwa nafasi ya 200 katika viwango vya fifa...

Wachaji wanao cheza ligi za mikoa watatoka wapi au ligi daraja la pili si kwenye mashindano haya haya....

Huyu Rais walio mchagua kwa kweli NI KANSA ya SOKA nchini mwetu..

Mashindano yanayo andaliwa na TFF yatakuwaje mazuri wakati hata ushawishi hayana..hiyo timu ya taifa ndo kabisaa wachezaji hawajitumi..
Nilitegemea rais atakuja kusema timu ya taifa iyandaliwe ya vijana tu wanao cheza mchangani wakati tunatengeneza mipango ya muda mrefu....

Ngoja turudi ULAYA
 
Chakushangaza hajiulizi kwanini Tanzania haijapata refa hata mmoja wa kuchezesha Chan. Yaani hadi CAF wamewabagua kwa ubabaishaji wao.
 
Verygood .....TFF.
Next step...... TFF taifisha vilabu vyenye mapato makubwa.
Baadae.......TFF wawe waendeshaji wa mashindano ya soka ya mashule na mashirika ya serikali na umma.
Halafu.......timu ya bunge ipangiwe ratiba.
then UMISETA na UMITASHUMTA vianze kuratibiwa na Rais wa TIFUTIFU

Aftazat TUNASHIRIKI WORLD Cup
 
Jicho la tatu katika kauli ya TFF japo sipingi mkuu ulichokiandika
Mpira wetu unahitaji kuwa chini ya usimamizi(monitor) kuanzia kwenye grass root..... Na usimamizi huo sio kwa ngazi za juu pekee La hasha, kuanzia huku kwenye ligi za kuku, mbuzi, Ng'ombe, jezi, mipira na hata mabonanza yanayohusisha mpira wa miguu.

Mashindano yanapokuwa kwenye usimamizi(Kibali) cha TFF kupitia mkoa na hata wilaya yanakuwa na shabaha kubwa katika Mambo mengi ya ukuzaji wa vipaji na mchezo wa soka kiujumla.
Kama usimamizi Bora na imara wa michuano, kuondoa ile dhana ya fujo katika michezo ya mchangani, kuondoa ile dhana ya vipaji kuishia huko baada ya mashindano, ila pia kurahisisha scouting kwa kwachezaji kutoka kwa wataalamu wa shirikisho kwaajili ya timu za vijana na timu nyingine.

Michuano inapotambuliwa inaandaa na kutambua Takwimu kwa wachezaji, waalimu husika pamoja na waamuzi katika career Yao.... Tunatatizo la utambuzi wa Takwimu(statistics) kwa wanamichezo wetu kuanzia chini, sababu ya usimamizi duni.

Kibali pia kitatoa uhalisia wa taarifa za mchezaji na kuondoa dhana inayotusumbua Sasa katika usajili wetu kwenye zile 10% za transfer fee baada ya mchezaji kuuzwa. Hapa wachezaji watakuwa kwenye kumbukumbu nzuri na za kueleweka.

Naunga mkono KIBALI kwa michezo ya mchangani almaarufu Ndondo.
 
Nyoosha Maelezo hawajakataza mashindano yoyote wanachosisitiza ni kuwepo na utaratibu maalum Wa kuandaa mashindano hya yawe na tija
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Nyoosha Maelezo hawajakataza mashindano yoyote wanachosisitiza ni kuwepo na utaratibu maalum Wa kuandaa mashindano hya yawe na tija
 
Back
Top Bottom