Hilo suala la shabiki wa Simba kuhudhuria games za Yanga na kinyume chake,mbona ni jambo la kawaida sana na lipo enzi na enzi? Nadhani mna stress fulani zinazowafanya muone hili jambo kuwa halikubaliki, nadhani ni kwavile hamjiamini.
Kuhusu mkao jukwaani; wewe unajua vyema kuwa pale uwanjani kuna (A)sehemu ya mashabiki wa Simba tu, (B)sehemu ya mashabiki wa Yanga tu, na (C)sehemu ya mashabiki mchanganyiko . Na hii kadhia mara nyingi inatokea hapo jukwaa C (maana hakuna shabiki mwenye akili timamu wa Simba anaweza kwenda jukwaa B, hali kadhalika wa Yanga kwenda jukwaa A, na kuanza kutukana - atakuwa hajipendi). Sasa ukiangalia kwa makini:migogoro imekuwa inatokea jukwaa 'C' sehemu ambayo yeyote anaruhusiwa kukaa na kutukana atakavyo. Sasa nyie mnataka ku-monopolize na jukwaa C? Mtakuwa na matatizo mahala.
Halafu eti unasisitiza;kwanini mtu aende kwenye mechi isiyomhusu? Hapo wala hata hakuna logic. Unataka kuniambia kwamba wikiendi ijayo Yanga hawatajitokeza kuishabikia Plateau United ya Nigeria? Kama juzi tu mlikuwa mnatoa unabii uliofeli dhidi ya Simba, na bado mmenunua jezi za Plateau mtashindwa kuibuka kwa Mkapa kuja kuizomea Simba?
Tunawakaribisha kwa Mkapa siku hiyo maana zomea zomea yenu ndo itatupa mzuka zaidi wa kuwaumiza hao Wanigeria wenzenu. Sisi hatutawafanyia vurugu ili mpate kujifunza somo la uvumilivu (tolerance) kuhusiana na kejeli za wapinzani kwenye soka.