TFF mnazilemaza Simba na Yanga kwa kuwaaminisha wamejitosheleza Kila eneo

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Leo TFF imetoa orodha ya Wachezaji na Walimu wanaowania tuzo mbalimbali za Ubora Kwa msimu wa 2022/2023. Ni Jambo jema linaloleta motisha Kwa Wachezaji na Walimu kuonyesha jinsi kujitoa kwao kunavyothaminiwa na mamlaka na Mashabiki wao pia.

Lakini kinachotia Shaka japo najua wapo watakaokuja kukejeli ni jinsi tuzo hizi zilivyojaa majina toka Simba na Yanga kuanzia Walimu hadi Wachezaji. Hali hii inazifanya timu hizi zijione zimekamilika wakati kiuhakika bado zina mapungufu hasa Kwa Wachezaji wa ndani àmbao wanazidiwa viwango na Wachezaji walioko timu ndogo.

Hata Kwa upande wa Wachezaji wa kigeni bado kuna timu za Kati zina Wachezaji Wana viwango vizuri na unhetamani kuwaona wakicheza timu kubwa badala ya waliopo. Katika vipengele vitano (5) Kati ya sita (6) vilivyowekwa ligi kuu (NBCPL) Makocha na Wachezaji wanatokea timu 3 tu za Simba, Yanga na Singida BS isipokuwa kipengele cha Chipukizi Bora mmoja tu anatokea Geita Gold na mwingine Coast Union.

Kama kweli huu ndo uhalisia basi maneno ya Ahmed Ally kwamba Ligi yetu ni dhaifu yalikuwa Sawa.


 
Kuondoa hii nashauri iandaliwe ligi yao maana hao wengine wasipojipanga itakuwa hivi hivi daima.
La sivyo kusiwepo kabisa na hayo mashindano ya TUZO.
 
Nenda ligi ya laliga kikosi bora kinatoka Madrid na Barcelona, nenda ligi ya Germany timu zinatoa wachezaji wengi ni bayern na dortmund na wengine kwaa mbali, nenda England vikosi vinatoka man City, Liverpool na wengine kwa mbaaali. Kwa maana yako unataka wachezaji watoke azam , geita, coastal, ruvu ???
 
Wewe tumia takwimu utaniambia kama huu ndo uhalisia. Na kama ndo uhalisia nasisitiza Ahmed Ally apewe maua yake nchi ina ligi ya timu 2.
Unahisi nani anasitahili kuingia toka hizo timu ndogo?, pia nani toka timu kubwa hasitahili kuwepo?.

Mpira siyo mchezo wa usawa , siku zote wanaofanya vizuri wanakuwa daraja lao la pekee yao.

Ukienda ligi zote duniani utakuta orodha kubwa ya tuzo inaelekea kwenye timu kubwa pekee za ligi hiyo
 
Kipre junior
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…