Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Leo TFF imetoa orodha ya Wachezaji na Walimu wanaowania tuzo mbalimbali za Ubora Kwa msimu wa 2022/2023. Ni Jambo jema linaloleta motisha Kwa Wachezaji na Walimu kuonyesha jinsi kujitoa kwao kunavyothaminiwa na mamlaka na Mashabiki wao pia.
Lakini kinachotia Shaka japo najua wapo watakaokuja kukejeli ni jinsi tuzo hizi zilivyojaa majina toka Simba na Yanga kuanzia Walimu hadi Wachezaji. Hali hii inazifanya timu hizi zijione zimekamilika wakati kiuhakika bado zina mapungufu hasa Kwa Wachezaji wa ndani àmbao wanazidiwa viwango na Wachezaji walioko timu ndogo.
Hata Kwa upande wa Wachezaji wa kigeni bado kuna timu za Kati zina Wachezaji Wana viwango vizuri na unhetamani kuwaona wakicheza timu kubwa badala ya waliopo. Katika vipengele vitano (5) Kati ya sita (6) vilivyowekwa ligi kuu (NBCPL) Makocha na Wachezaji wanatokea timu 3 tu za Simba, Yanga na Singida BS isipokuwa kipengele cha Chipukizi Bora mmoja tu anatokea Geita Gold na mwingine Coast Union.
Kama kweli huu ndo uhalisia basi maneno ya Ahmed Ally kwamba Ligi yetu ni dhaifu yalikuwa Sawa.