TFF msameheni Manara

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ukweli ni kuwa mkubwa hakosei. Rais wa TFF ni mtu mkubwa sana kwenye mpira wetu Tanzania. Ndiye kioo Cha mpira wetu kwasasa, yaani kama ni ukatoliki yeye ndiye wa kanisa nchini na kama ni uislamu yeye ndiye Mufti wetu, haifai atokee mtu yeyote miongoni mwetu akamdhihaki hata kwa kutania TU akiwa anafuraha au ana hasira ya kitu chochote kinachohusu mpira wetu wa miguu.

Ni kweli Yanga ni kubwa kuliko coastal Union, mwenendo wa matokeo ya mechi Ile ya final ya Azam ulikuwa unaiduwaza Yanga kabla ya Yanga kupindua matokeo dakika za mwisho za mechi na kuibuka mabingwa. Furaha ya kupindua matokeo iliwafurahisha wadau wengi wa Yanga kiasi Cha kuwageuza wendawazimu (euphoric) wa muda kiasi Cha kujisahau kuwa Kuna maisha baada ya Ile mechi. Haji Manara alikuwa miongoni mwa wadau hao waliozidisha furaha na uendawazimu wa mpira siku ile kiasi Cha kwenda kukabiliana na kiongozi/Kadinali/mufti wake kwenye mpira, haikuwa sawa hata kama rais nae alionekana kufurahia mafanikio ya coastal Union kama mdau wa coastal Union pengine na Simba.

Binafsi ninamuona Manara kama mtu aliyeingizwa mtegoni na Ile comeback ya Yanga iliyopatikana kwa miujiza na bahati TU badala ya ubora wa kikosi.

Watalaam wa afya ya akili Wana kitu wanachokiita pre-morbid personality, yaani tabia ya mtu kabla ya kupata tatizo/kuugua. Haji maisha yake ameyawekeza zaidi kwenye soccer kiasi Cha kupitiliza, hivyo ufahamu wake na mahaba yake kwenye mpira ni makubwa zaidi kuliko watu wengi.

Mpira ndicho kitu pekee kinachofidia ulemavu wake alionao, na Kuna walemavu wengine kama yeye ambao wanapata nguvu zao kwa kumtazama Manara na kazi zake na mafanikio yake kama mlemavu mwenzao (role model)

Hivyo, kwa maslahi mapana ya mpira, Manara, walemavu na hata wadau wa mpira, nataka kuamini kuwa Haji amejifunza kutokana na kosa lake, ndio maana amekuwa akiomba radhi kila mtu baada ya pale.
TFF itakuwa imara sana kitaifa na kimataifa kama itaamua kumsamehe Manara badala ya kumfungia miaka 2 na kulipwa 20m na mlemavu. Haji hawezi kusukuma mkokoteni juani kama wengine. Ukimgungia mpira atafanya kitu gani kingine?

Ni mawazo yangu TU kama mdau wa mpira.
 
Sheria ikitekelezwa ipasavyo, kila mtu araheshimu na kutakua na mipaka. Lakini ikifanywa kwa mihemko basi itaonekana kama shamba la bibi, kila mmoja ataivunja makusudi maana anajua atakuja kusamehewa. Acha ajifunze ili na wengine waheshimu kanuni na taratibu zilizowekwa. Vinginevyo tutakua kama mpira wa mchangani.
 
TFF toka ianzishwe imeshafungia maisha wadau wengi wa soka, Shaffiih dauda aka digala alifungiwa asijihusishe na soka na ukitazama yy alikuwa na wadhifa mkubwa DRFA na ndie mwanzilishi wa ndondo cup ila TFF haikumuonea huruma,akala nyundo zake iweje leo hii kuwe na double standard ktk kuhukumu? Yaani manara aachwe huru huku kina dauda waendelee kutumikia vifungo vyao? Au kila mtu aliyefungiwa na TFF apewe msamaha na afutiwe hukumu?
 
Kanuni ipi imevunjwa?
 
Huwezi kumsamehe mtu ambaye daily anampiga vijembe karia

Saizi katengeneza sumu kwa mashabiki wa Yanga na kweli wamekuwa poisoned wameanza kuiita Simba TFF
Kwanini TFF haikuonekana kwenye siku ya wananchi? Kwanini Yanga haikualikwa mkutano wa Caf? Kwanini Yanga inayosafiri kwenda Arusha itangulie kucheza na polisi wakati Simba isiyosafiri ichelewe kucheza mechi yake, baada ya Yanga kucheza?
 
Mimi naomba tu nikurekebishe kwenye hicho cheo cha juu cha ukatoliki nchini! Kwa ufupi tu ni kwamba, rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ndiye mwenye mamlaka makubwa kuliko hata huyo Kardinal! Maana yeye huchaguliwa na Maaskofu wote wa Katoliki nchini kushika hiyo nafasi.

Cheo cha Ukardinali kinatumika zaidi Vatican, Italy ambapo Makardinali wakioteuliwa na Papa hutumika kama washauri wake wa karibu katika masuala mbalimbali! Yaani Makardinali ni kama Mawaziri/Maparoko vile kule Vatican, halafu Papa ni Rais/Askofu wa Vatican.

Kardinali anaweza kuwa hata Padre tu wa kawaida! Muhimu tu ateuliwe na Papa katika hiyo mafasi. Hivyo si kweli kama Kardinali ndiye Mkuu wa Kanisa Katoliki kwenye nchi. Mfano kwa Tanzania; rais wa sasa wa TEC Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga ndiye bosi wa Maaskofu wengine!


Ukitoka hapo unakuja kwa wale Maaskofu wa Majimbo mkuu mfano DSM, Mbeya, Dodoma, Arusha, Mwanza, nk. Then unakuja kwa Maaskofu wa kawaida wa Majimbo mfano Mahenge, Ifakara, Tunduru Masasi, Lindi, Geita, nk. Naamini umenielewa.
 
Makosa ni tofauti na sababu zake ni tofauti pia
 
Elimu tosha hii, ahsante.
 
Akisamehewa manara wafungwa wote magerezani waachiwe itakua haina maana ya kuwepo hata magereza yenyewe sasa
 
Kwanini TFF haikuonekana kwenye siku ya wananchi? Kwanini Yanga haikualikwa mkutano wa Caf? Kwanini Yanga inayosafiri kwenda Arusha itangulie kucheza na polisi wakati Simba isiyosafiri ichelewe kucheza mechi yake, baada ya Yanga kucheza?
Nendeni mkalalamike kwa Karim Boimanda na Almas kasongo kwani wakati TPLB wanatoa fixtures za msimu mpya ,ninyi crying babies mlikuwa wapi?
 
Tatizo la Manala ni kujikweza kupita kiasi.
Angejishusha akaomba radhi au kukata rufaa angeweza kusamehewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…