TFF msameheni Manara

TFF msameheni Manara

Ukweli ni kuwa mkubwa hakosei. Rais wa TFF ni mtu mkubwa sana kwenye mpira wetu Tanzania. Ndiye kioo Cha mpira wetu kwasasa, yaani kama ni ukatoliki yeye ndiye Kadinali na kama ni uislamu yeye ndiye Mufti wetu, haifai atokee mtu yeyote miongoni mwetu akamdhihaki hata kwa kutania TU akiwa anafuraha au ana hasira ya kitu chochote kinachohusu mpira wetu wa miguu.

Ni kweli Yanga ni kubwa kuliko coastal Union, mwenendo wa matokeo ya mechi Ile ya final ya Azam ulikuwa unaidiwaza Yanga kabla ya Yanga kupindua matokeo dakika za mwisho za mechi na kuibuka mabingwa. Furaha ya kupindua matokeo iliwafurahisha wadau wengi wa Yanga kiasi Cha kuwageuza wendawazimu (euphoric) wa muda kiasi Cha kujisahau kuwa Kuna maisha baada ya Ile mechi. Haji Manara alikuwa miongoni mwa wadau waliozidisha furaha na uendawazimu wa mpira siku ile kiasi Cha kwenda kukabiliana na kiongozi/Kadinali/mufti wake kwenye mpira.

Binafsi ninamuona kama mtu aliyeingizwa mtegoni na Ile comeback ya Yanga iliyopatikana kwa miujiza na bahati TU badala ya ubora wa kikosi Chao. Watalaam wa afya ya akili Wana kitu wanachokiita pre-morbid personality, yaani tabia ya mtu kabla ya kuipata tatizo husika. Haji maisha yake ameyawekeza zaidi kwenye soccer kiasi Cha kupitiliza.

Mpira ndicho kitu pekee kinachofidia ulemavu wake alionao, na Kuna walemavu wengine kama yeye wanapata nguvu zao kwa kumtazama Manara na kazi zake na mafanikio yake kama mlemavu mwenzao.

Hivyo, kwa maslahi mapana ya mpira, Manara, walemavu na hata wadau wa mpira nataka kuamini kuwa Haji amejifunza kutokana na kosa lake, ndio maana amekuwa akiomba radhi kila mtu baada ya pale. TFF itakuwa imara sana kama itaamua kumsamehe Manara badala ya kumfungia miaka 2 na kulipwa 20m na mlemavu.

Ni mawazo yangu TU kama mdau wa mpira.
Ungekuwa na akili usingeandika huu utetezi.

Manara ni nani ktk Sola la Tz?

Kwani bila Manara soka halitaendelea?
 
Unampa mtu msamaha leo kesho anatoka kwenye media kukusagia kunguni?
Sema tu manara kapanda mtumbwi wa vibwengo
 
Lile wenge lenu la Manara mkubwa zaidi ya TFF naona limekwisha, sasa subirini atandikwe, nashangaa TFF bado wapo kimya mpaka leo sijui tatizo nini.
 
Mimi naomba tu nikurekebishe kwenye hicho cheo cha juu cha ukatoliki nchini! Kwa ufupi tu ni kwamba, rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ndiye mwenye mamlaka makubwa kuliko hata huyo Kardinal! Maana yeye huchaguliwa na Maaskofu wote wa Katoliki nchini kushika hiyo nafasi.

Cheo cha Ukardinali kinatumika zaidi Vatican, Italy ambapo Makardinali wakioteuliwa na Papa hutumika kama washauri wake wa karibu katika masuala mbalimbali! Yaani Makardinali ni kama Mawaziri/Maparoko vile kule Vatican, halafu Papa ni Rais/Askofu wa Vatican.

Kardinali anaweza kuwa hata Padre tu wa kawaida! Muhimu tu ateuliwe na Papa katika hiyo mafasi. Hivyo si kweli kama Kardinali ndiye Mkuu wa Kanisa Katoliki kwenye nchi. Mfano kwa Tanzania; rais wa sasa wa TEC Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga ndiye bosi wa Maaskofu wengine!

Ukitoka hapo unakuja kwa wale Maaskofu wa Majimbo mkuu mfano DSM, Mbeya, Dodoma, Arusha, Mwanza, nk. Then unakuja kwa Maaskofu wa kawaida wa Majimbo mfano Mahenge, Ifakara, Tunduru Masasi, Lindi, Geita, nk. Naamini umenielewa.
Amina

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Afungiwe tu maisha ili kukomesha uchawa ktk soka..ili atafute kazi nyingine afanye
 
wache ajifunze adabu kwanza ili next time awe makini - si watu wote wa kuparamia paramia.
 
Tatizo la Manala ni kujikweza kupita kiasi.
Angejishusha akaomba radhi au kukata rufaa angeweza kusamehewa.
Kujikweza ni tabia ya viumbe wote wanaojiona kuwa ni dhaifu mbele ya wengine, hivyo wanapewa na mwenyezimungu tabia itayofidia udhaifu wa maumbile yao. Mfano, viumbe wenye umbo dogo porini wananguruma kwa sauti kubwa kuwatisha wengine kwa sauti zao, wengine wanakuwa na sumu Kali, wengine wanakimbia sana, wengine wanapewa hafuru mbaya. Watu wafupi na maumbile madogo huwa wanaongea na kucheka sana, kuvaa suti na macheni shingoni nk. Kwavyovyote vile tabia ya Haji inamsadia sana kuziba udhaifu wa ngozi na macho aliopewa na mwenyezimungu. Kwani jamii imezoea kuwaona watu wenye ualbino kama wanyonge, maskini, tegemezi, wanaokufa mapema, nk. Hivyo tusishangae sana kuwaona watu wenye ulemavu wa viungo wakiwa na nguvu sana kwenye viungo vingine kama mdomo, mikono, miguu, brain, nk, hii ni mwenyezimungu anawafidia kile alichowapunguzia.

Haji kwa maumbile yake hawezi kwenda kusukuma mkokoteni juani, unapomfungua kazi yake ya kusema kwa miaka 2 na kutaka akulipe 20m sio sawa, na Mungu lazima atakuadhibu TU hapahapa duniani, upende usipende. Pale Simba walimdhulumu mlemavu (Manara) wakajuta hasara waliyoipata kwa kuondoka Haji. Mungu sio mjinga kwa kiasi hicho TFF wanavyomuona mlamavu Haji.

Kila anaemdhihaki mlemavu, mjane na mtoto Mungu hamuachi salama.
 
Huwezi kumsamehe mtu ambaye daily anampiga vijembe karia

Saizi katengeneza sumu kwa mashabiki wa Yanga na kweli wamekuwa poisoned wameanza kuiita Simba TFF
Kwenye hii adhabu TFF itapingana na kila mtu duniani anaewaonea huruma walemavu, except baadhi ya mashabiki wa Simba
 
wache ajifunze adabu kwanza ili next time awe makini - si watu wote wa kuparamia paramia.
Hakuna mkamilifu, ni kosa la kimichezo TU kwa wanamichezo waliokutana mchezoni,
 
Tatizo la Manala ni kujikweza kupita kiasi.
Angejishusha akaomba radhi au kukata rufaa angeweza kusamehewa.
Huo ndio ukweli.

Anaweza kuomba msamaha leo, Kesho anarudi kivingine - Ana uthubutu wa kuwawekea Kibesi wenye mamlaka (Rais wa TFF na Waziri).
Mbaya zaidi ni kwamba matatizo yake ya mtindio wa ubongo anayafanya kuwa ni matatizo ya Club
 
Huo ndio ukweli.

Anaweza kuomba msamaha leo, Kesho anarudi kivingine - Ana uthubutu wa kuwawekea Kibesi wenye mamlaka (Rais wa TFF na Waziri).
Mbaya zaidi ni kwamba matatizo yake ya mtindio wa ubongo anayafanya kuwa ni matatizo ya Club
Ni kanuni ipi ya mpira wa miguu ya TFF ameivunja inayomtaka alipe 20m na kufungiwa miaka 2?
 
Back
Top Bottom