TFF mtuache tumalize uchaguzi mkuu wa rais

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
TFF msije kusema hamukuambiwa, Mechi ya Simba na Yanga kuchezwa tarehe 18/10/2020 siku 9 kabla ya siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaofanyika tarehe 28/10/2020 hapa kuna jambo litazua jambo!

Machungu yanayotokana na hizo Mechi za watani yana athari zinazodumu kwenye jamii kwa kipindi fulani baada ya mechi. Kuna Uharibifu wa Mali, Kuna viffo vya msutuko, Kuna malalamiko ya Upendeleo wa timu fulani, Kuna maazimio ya Kutimuana, Kuna Kususiana, Kuna kuona aibu na kufanya mtu akae ndani tu kwa aibu ya kufungwa nk nk nk nk.

Kwa muktadha huu na kwa kuzingatia Uwepo wa Mechi za Kimataifa za Kirafiki ni wazi kabisa kwamba TFF hawanabudi kubadilisha tarehe ya Mechi husika ili kupisha Zoezi la Uchaguzi Mkuu. Kuna kundi linaweza kususa au kununa likajitokeza kwa Uchache kwenye Uchaguzi Mkuu.

Nawasilisha.
 
Siku tatu baada ya mechi ya Tarehe 18, kuna mfadhili mmoja atakua kwenye wakati ngumu na mwishoe ata Susa Kama alivyo Susa baada ya mechi na mtibwa kule Zanzibar. Ni Jambo la muda tu.

Nyie mnapaswa kujua kuwa binti akiolewa na kuingizwa chumbani kwa mumewe basi hana jinsi tena...jipurukusheni kadri mnavyoweza lakini 18 tunaenda kumuenzi Mkapa
 
Balaa zito linakuja! naona mafuriko yanainyemelea Jangwani.
 
Mimi yanga .. ukweli tumesajili na timu yetu imeongezeka ubora kuliko yanga ya msimu uliopita..

Mpira ni mchezo wa wazi.. macho yanga yametizama yanga ya sasa hivi na simba ya sasa hivi ikoje.. akili yangu na macho yangu yananiambia yanga bado hatujawafikia mikia kwa ubora wa wachezaji.. tarehe 18 yanga tutashinda kwa mbinu kali.. ila tukiseme tucheze kawaida bila mbinu za aston villa kwa liverpool mikia watatufunga tena nyingi
 
mleta uzi bila shaka ni mshabiki kindaki ndki wa utopolo sasa wanaanza kusingizia uchaguzi baada ya liva man u na man cty timu nyingine kubwa inayofuatia hapo kwa kufungwa goli nyingi kwenye mechi moja ni yanga 5 zinawahusu
 
Yanga mnatafuta sababu mapema ili mseme hamjajiandaa ,na mnataka mechi isogezwe ili mjiandae .
Ratiba ilishapangwa hakuna haja ya kusingizia uchaguzi mechi lazima ichezwe .
Halafu kusiwe na haja ya kumleta Magufuli uwanjani wakati huu wa uchaguzi ni kupiga kampeni, kama Magufuli atakuja uwanjani basi na Lissu awepo
 
Hivi kwanini mnawadharau na kuwakera Sana yanga?
Yanga tayari wamewa tag TFF wasome hili bandiko ili kocha mpya ajaye apate Chemistri ya Kikosi chake kipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…