TFF na Bodi ya ligi inawakingia kifua marefa wanaochezesha hovyo kwa kuwapiga faini wakosoaji

TFF na Bodi ya ligi inawakingia kifua marefa wanaochezesha hovyo kwa kuwapiga faini wakosoaji

Nimeshangazwa na hii habari iliyoandikwa na ukurasa wa mtandao wa mwananchi kuona Ally kamwe kupigwa faini.

"Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe ametozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la kumkejeli na kumdhalilisha mwamuzi wa mechi ya Singida Big Stars dhidi ya Simba kupitia mtandao wa kijamii.

"Baada ya kumalizika kwa mechi, Ali Kamwe aliweka chapisho katika ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ambalo lilikuwa na picha ya mwamuzi (Malogo) huku akiunganisha na wimbo wa msanii wa muziki kizazi kipya, Billnass uitwao Maokoto, hali iliyoleta tafsiri ya kumhusisha mwamuzi huyo na masuala ya fedha ama rushwa," imeeleza taarifa ya Bodi ya Ligi"

Kama TFF na Bodi ya ligi inawapiga faini wakosoaji je hao marefa wanapewa adhabu gani kwa utumbo wanaoufanya uwanjani?

Kama hatutaona kufungiwa au faini kwa marefa waliochezesha mechi ya Dodoma fc vs Azam Fc na Refa Tatu Malogo aliyechezesha mechi ya Singida fountain Gate Fc dhidi ya Simba sc Basi tulio welevu kama NALIA NGWENA tutajua kuwa TFF na Bodi ya ligi inahusika kwa asilimia Mia kuwatuma marefa wachezeshe kwa maelekezo maalumu.
Hakika MACHOKO hamtaisha Nchi hii
 
Back
Top Bottom