TFF na bodi ya ligi mnamwachaje Ahmed Ally mmezikubali kauli zake?

kambale mnene

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
271
Reaction score
197
Inanipa shida kauli ya msemaji wa simba, aliposema ligi yetu ni dhaifu.
Pia zinanipa shida Tff na bodies ya ligi wenye mamlaka na ligi yetu.

Ligi haiwezi kuwa dhaifu kama muandaaji na msimamizi ni imara. Kwa maana hiyo kwa kauli ya msemaji wa simba,Tff na bodi ya ligi ni dhaifu.

Linitazamia msemaji huyo angekwisha hojiwa na ingebidi aadhibiwe. Mfano ukisema chakula ni kichafu, maana yake muandaaji wake pia ni mchafu.

TFF NA BODI YA LIGI MSIPOCHUKUA HATUA KWA MSEMAJI WA SIMBA,WAPENDA MPIRA WA MIGUU TUTAKUBALIANA NAYE KUWA NINYI NI DHAIFU.
 
Hata uliyeandika nawe ni dhaifu!
 
Ligi inachezwa kwenye viwanja kama majaruba ya mpunga halafu wewe unaiona ligi ni bora.

Ligi inayochezwa kwenye viwanja aina ya Manungu, Sokoine, Karume, Nelson Mandela hiyo ligi ni dhaifu.

TFF kuwafungia waamuzi mbalimbali ni uthibitisho pia kuwa ligi ni dhaifu kwa upande wa waamuzi.
 
Bado ni dhaifu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…