TFF na Bodi ya ligi Tanzania, tukisema kuwa ratiba yenu ni kandamizi (uonevu) kwa Yanga sc tutakua tumrkosea??

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Mpaka Sasa NALIA NGWENA nimechoka sana, nilipochungulia ratiba ya Yanga kumaliza msimu ni ngumu sana Tena sana.

Tarehe 03/6 Yanga itacheza mchezo mzito Tena wa kufa mtu(fainali huko Algeria)

Tarehe 06/06 Yanga anakutana na Mbeya city huko mbeya

Tarehe 09/06 Yanga atakutana Tanzania prisons

Tarehe 12/06 fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Azam FC. Hii ni fainali Tena mechi ngumu mno.

NALIA NGWENA nawauliza TFF na Bodi ya ligi nchini hapa kipindi mnapanga hii ratiba mlijua Yanga inachezesha maroboti ya Elon musk??

Au kwa kua mmeona timu yenu pendwa (Simba sc) imekosa hata kombe la kufutia machozi mmeamua kuikomoa Yanga sc??

Nawasilisha hoja.
 
Kwahio umesahau ka mnakikosi kipana, au mnaanza kujihami? mpigwe tu nyingi na mwarabu then azam awazike kabisa.
 
Kumbuka timu Ina safiri hiyo Ina pumnzika saa ngapi??
Inasafiri Kwa Miguu?hapo hiyo fainali tu ndio kikosi Cha Kwanza,hao akina mbea city sijui kikosi no 2 kitahusika.
 
Mmeanza kutafuta wachawi kabla ya kukandwa na kukosa Looosers Cup. Mwaka huu mtalaumu wote kuanzia mpishi wenu mpaka Feisal
 
Inasafiri Kwa Miguu?hapo hiyo fainali tu ndio kikosi Cha Kwanza,hao akina mbea city sijui kikosi no 2 kitahusika.
Unaipangia yanga iingize kikosi gani au hao Tff ndiyo wamepanga kwa kutazama kuwa Yanga itapumnzisha wachezaji??
 
Mechi ya muhimu hapo ni hiyo fainali ya Azam federation ambayo ni ya mwisho. Mechi zilizobaki za ligi kuu Yanga hata akiwapanga kikosi B ni sawa tu maana ubingwa wameshabeba
 
Mmeanza kutafuta wachawi kabla ya kukandwa na kukosa Looosers Cup. Mwaka huu mtalaumu wote kuanzia mpishi wenu mpaka Feisal
Jikite kwenye hoja siyo unaleta ushabiki maandazi
 
Mechi ya muhimu hapo ni hiyo fainali ya Azam federation ambayo ndio inayoanza kabla ya mechi zingine. Mechi zilizobaki za ligi kuu Yanga hata akiwapanga kikosi B ni sawa tu maana ubingwa wameshabeba
Kwa hiyo unataka kusema kuwa hata TFF nao wamepanga ratiba kwa kuangalia kuwa watapumnzisha wachezaji
 
Na pia ukiangalia kwa mpangilio wa muda wa kupumzika upo sawa tu kikanuni. Ulaya timu inacheza jumamosi, jumanne inacheza tena
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa hata TFF nao wamepanga ratiba kwa kuangalia kuwa watapumnzisha wachezaji
Mkuu hapo hakuna kanuni iliyovunjwa hata ulaya timu zinapimzika siku mbili tu ya tatu wanakipiga mechi tena. Mbona ni kawaida tu ila kwavile Tanzania timu zimezoea kudekeshwa ndio tunashangaa ratiba kama hii. Kama sikosei msimu uliopita au msiimu wa nyuma yake, Simba walipangiwa ratiba kama ya namna hii. Tuache kulalamika kwa vitu visvyovunjwa kanuni za mpira.
 
Mbona ratiba ipo vizuri kabisa masaa 72 ya kupumzika

Ukichangia na kikosi bora na kipana mlichonacho sikutegemea hivi vilio
Masaa 72 kwa Ulaya, unategemea miundombinu ya Tanzania utoke mbeya ukacheze Tanga na ufanye mazoezi ni sawa?
 
Mbona ratiba ipo vizuri kabisa masaa 72 ya kupumzika

Ukichangia na kikosi bora na kipana mlichonacho sikutegemea hivi vilio
Yaani kutoka Algeria ktk Fainali tarehe 03, game inachezwa saa nne usiku kwa saa za huku ...asubuhi tarehe 04 safari kuja Dar...watue waunganishe Ndege mpaka mbeya....hiyo miili ni ya chuma !? Mbeya wataingia saa ngapi!? Watafanyia mazoezi siku Moja then siku inayofuata mechi!!!?


Umbali wa kusafiri na uchovu wa mechi ya Fainali hamuuoni!?
 
Masaa 72 kwa Ulaya, unategemea miundombinu ya Tanzania utoke mbeya ukacheze Tanga na ufanye mazoezi ni sawa?
Yanga hii ya tajiri asiye bahili GSM hilo siyo tatizo kabisa acha kulialia mkuu Yanga itaenda mbeya wataacha ndege yao airport mchezo ukiisha wananyanyuka wanarudi avic town wanafanya zoezi kesho yake wanapanda mwewe hao Tanga ha ha ha
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…