TFF na Bodi ya Ligi wanapaswa kupanga mikakati maalumu ya kuzuia mashabiki kukaa sehemu hatarishi kama juu ya miti wanapokua wanatazama timu zao

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Shabiki ni mchezaji wa kumi na mbili (12) Kama kanuni za mpira zinavyosema, hivyo basi TFF na Bodi ya ligi inapaswa kuwalinda mashabiki kwa kutengeneza mikakati maalumu.

Kumekua na kasumba (tabia) ya mashabiki Kupanda juu ya Miti au kwenye minara huku wakishuhudia timu zao na kukaa huko mpaka dakika tisini kutamatika.

Mashabiki hawajali kama hayo maeneo ni hatari kwa afya zao na bila kujali kuwa mpira ni hisia timu yake inaweza kufungwa na kukosa nguvu akaanguka au anaweza kuona timu yake imeafunga bao na kushangilia kwa hisia na kupelekea kuanguka chini na Kuumia au kupoteza maisha kabisa.

Upandaji wa kwenye minara, Miti na Miamba mirefu huwa nauona sana sana kwa mashabiki wa Simba sc na Yanga haswa wanapocheza Mechi za mikoani.

Maoni Yangu: TFF na Bodi ya ligi inapaswa kutengeneza mikakati maalumu ili kudhibiti tabia Kama hii kwa mashabiki wanaohatarisha maisha Yao.

 
Kipato chenyewe kinazingua Kama umeme wa bwawa la Nyerere.
Pesa ya kulipa getini tutapata wapi??
KAA NYUMBANI UTAZAME KWENYE TV NA SIYO KUJA KUPANDA JUU YA MTI UKIFA FAMILIA YAKO ATALEA NANI?!
 
Ukishabikia sana simba na yanga Automatically kichwani zinaanza kulegea.

Nawasihi sana watanzania wenzangu, Hizo timu ni mtego wa kisiasa wa propaganda za Dola.

Msipoteze sana Muda kwenye mambo za simba na yanga.

MWENYE MASIKIO YA KUSIKIA NA ASIKIE
 
AHSANTE SANA MAMA USHAURI[emoji2935]
 
Naunga mkono hoja.
 
Siyo kazi ya Bodi ya ligi, Ni watu wa Uwanja na Usalama
 
Sijawahi kuona hata wakikemea hili jambo. Huwa tunasubiri mtu afe kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…