NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,587
- 13,425
Shabiki ni mchezaji wa kumi na mbili (12) Kama kanuni za mpira zinavyosema, hivyo basi TFF na Bodi ya ligi inapaswa kuwalinda mashabiki kwa kutengeneza mikakati maalumu.
Kumekua na kasumba (tabia) ya mashabiki Kupanda juu ya Miti au kwenye minara huku wakishuhudia timu zao na kukaa huko mpaka dakika tisini kutamatika.
Mashabiki hawajali kama hayo maeneo ni hatari kwa afya zao na bila kujali kuwa mpira ni hisia timu yake inaweza kufungwa na kukosa nguvu akaanguka au anaweza kuona timu yake imeafunga bao na kushangilia kwa hisia na kupelekea kuanguka chini na Kuumia au kupoteza maisha kabisa.
Upandaji wa kwenye minara, Miti na Miamba mirefu huwa nauona sana sana kwa mashabiki wa Simba sc na Yanga haswa wanapocheza Mechi za mikoani.
Maoni Yangu: TFF na Bodi ya ligi inapaswa kutengeneza mikakati maalumu ili kudhibiti tabia Kama hii kwa mashabiki wanaohatarisha maisha Yao.