TFF na Jemedali Said wana uhusiano gani?

TFF na Jemedali Said wana uhusiano gani?

TFF ni chombo cha umma na kinachominiwa ndani na nje ya nchi. Jemedari Said anasema kuwa ana uhakika na vyanzo vyake vya habari ambazo zinahifadhiwa TFF. Ni mfanyakazi gani ndani ya TFF ambae anampa Jemedari habari binafsi za watu na taasisi zinazozua taharuki kwa umma? Tuna wasiwasi na TFF na hatuna imani nayo kwenye hili, Kwanini kwa mfano habari za Juma Mgunda na Nabi zianze kumfikia Jemedari kabla ya umma wa wanamichezo na badala ya taasisi zenyewe?

Kidau na huyo jemedari walicheza mpira pamoja kuke kariakoo
 
Tatizo lako unadhani mpira ni Serikali au taasis ya umma ,hata Fifa vitu vinavyoendelea ukitaka kuvijua unaenda kwenye page za waandishi wabobevu wa habari za michezo unapata tetesi ,mashirikisho ya mpira sio vyama vya siasa jifunze ,hakuna confidentiality unayoitaka haipo
Wacha ujinga, yaani kuwakalia uchi wafanyakazi wa TFF wakuvujishie taarifa.
Tatizo lako unadhani mpira ni Serikali au taasis ya umma ,hata Fifa vitu vinavyoendelea ukitaka kuvijua unaenda kwenye page za waandishi wabobevu wa habari za michezo unapata tetesi ,mashirikisho ya mpira sio vyama vya siasa jifunze ,hakuna confidentiality unayoitaka haipo
Aliyekwambia TFF ni kijiwe binafsi nani? Kama sio taasisi ya umma waulize akina Malinzi waliokamatwa na dola kwenda ndani kwa ubadhilifu wa hela za TFF
 
Naomba hako kapicha please......
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Screenshot_20220915-211720_Opera%20Mini.jpg
 
Kumbe huyu ndo jemedari mwenyewe?
Huyu jamaa anawaza negative all the time kuhusu Yanga, ataumia bure kwakuwa Yanga ni taasisi kubwa kuliko hata CCM, hataweza kushindana nayo kwa kila kitu. Ndani ya maamuzi ya Yanga wako wadau mbalimbali kutoka sekta tofautitofauti zikiwemo ofisi ya Rais, Bunge, mahakama, vyama vya siasa, mawaziri, wabunge, usalama wa taifa, polisi, wafanyabiashara na watu binafsi wengi sana. Yanga na Simba sio vijiwe vya kihuni ambavyo mtu mmoja anaweza kupambana navyo na kuvishinda. Utaudhi watu wengi sana wenye nafasi mbalimbali, jinsia, dini na elimu tofauti. Huwezi kushinda kama utatanguliza chuki maana Simba na Yanga ni kama watoto mapacha, hivyo hata utani wetu lazima uwe na kiasi ili usichanganye na chuki zako binafsi. Maana hakuna mtu mmoja hata akiwa nani kwenye nchi hii anaweza kuihujumu Simba au Yanga akafanikiwa na kubaki salama.

Kuna siku moja nimewahi kumwambia Manara humu humu kuwa sio kila wakati lazima uitaje Simba vibaya kwa maslahi yako na ugomvi wako binafsi na Simba, maana Simba ni zaidi ya Babra na Mo.
 
Back
Top Bottom