MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Baada ya kuangalia game ya Kongo DRC vs Uganda imenipa tafakari kubwa sana. Ilikuwa game ya viwango ambayo hata kama Taifa Stars tungeingia na akina Samatta ingekuwa aibu.
Kwanini pamoja na ligi yetu kuwa bora kwa udhamini kuongezeka by far kulinganisha hizi nchi jirani lakini bado hatuzalishi wachezaji bora? Uganda wamechukua wachezaji wengi wa Vipers lakini uwezo wao ni mkubwa mno hata kuwadhibiti Wakongo.
Hapa Tanzania timu zetu zote kubwa bila International players pengine hata ubingwa wa ndani ungekuwa rehani. Kipi hakiwekwi wazi kinachokwamisha kupata quality players. Imagine ilifikia hatua Nyoni na Yondani waliombwa wasistaafu timu ya Taifa kutokana na uhaba wa mabeki wa kati kipi kile!
Issues za sports academy imesemwa sana ila hata hizi zilizopo zinakwama wapi? Zimetoa wachezaji competitive enough kama mfano kwa Taifa? Ndio wapo ila kawaida! Simba imehangaika kutafuta kiungo mkabaji na locally hakuna mchezaji bora aliyewafaa wa kumpiku walau Erasto Nyoni! Yanga pale wamemsajili Mudathir lakini bado bila Bangala na yule mganda hawatoboi. Why?
Nafikiri Serikali ikubali kurudisha mashindano ya shule za msingi na sekondari kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa. Hizi gharama wasikwepe tena ipitishwe bungeni. Watoto karibia wote wapo huko mashuleni, hakuna mbadala wa kupata vipaji zaidi ya huko.
Wadau wa michezo hasa watangazaji pia watengeneze ajenda zitazosaidia michezo badala ya vipindi vyao kutawala trending Issues tena gossips. Ni aibu nchi kuwa na michuano mbadala tegemeo kama Ndondo cup tena juhudi za mtu binafsi badala ya mikakati ya kitaifa.
Sasa Wakongo, wazambia n.k wanakimbilia Tanzania ambako ushindani wa local players upo chini sana. Hatuandai wachezaji bora, hatuna mikakati ya kuandaa makocha bora alafu kesho Taifa Stars ikicheza tunahamasishana kutegemea miujiza!
Tubadilike...