TFF ndio chanzo cha uharibifu wa miundombinu Uwanja wa Taifa

TFF ndio chanzo cha uharibifu wa miundombinu Uwanja wa Taifa

avalanche

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
227
Reaction score
234
Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu hivi kwanini vilabi vya Simba na Yanga mpaka leo havina viwanja vyao binafsi?? Namshukuru Mungu kuwa nimepata kuelewa kuwa hizi timu zimehujumiwa na TFF pamoja na mashirikisho ya soka yaliyopita huko nyuma kama FAT na mengineyo yaliyokuwepo tangia hizi klabu kongwe zianzishwe miaka ya 1930.

Hizi ni klabu ambazo kwa sasa zilitakiwa kila moja iwe hata na viwanja viwili viwili, vya mashabiki na vya mazoezi. Lakini matokeo yake mpaka hivi sasa ndio vimeanza kutafuta maeneo ya kujenga viwanja vyao vya mazoezi. Hizi taasisi zilizokuwa na dhamana ya kusimamia mpira wa miguu kipindi hiko chote, yanaelewa kuwa hivi vilabu vikiruhusiwa kuwa na viwanja vyao wenyewe na usimamizi wa mechi kubwa pindi zinapokutana, pesa hazitoangukia mikononi mwao kama ilivyo sasa katika uwanja wa taifa.

Sioni mantiki ya kuendelea kutumika uwanja wa taifa mpaka unafikia hatua ya kuharibiwa na mashabiki, uwanja ambao ulijengwa kwa pesa zetu wenyewe walipa kodi, sababu tu ya mihemko ya upenzi wa vilabu. Waviachie vicheze kwenye viwanja vyao uone kama uharibifu huu ungetokea.

Leo Azam wananyimwa haki kutumia uwanja wao wa nyumbani kwa mechi zake za nyumbani sababu tu TFF wanajua watakosa pesa kuneemesha matumbo yao, hii inakatisha tamaa vilabu vyetu kuongeza wigo wa mapato yake kwa mechi ambazo zingechezewa kwenye viwanja vyao.

Nitazidi kuilaumu TFF kwa uharibifu wa viti sababu pia hawakuweka usimamizi wa kutosha kuhakikisha uwanja una hali ya usalama, badala yake macho yao yote yakaelekezwa kwenye ukusanyaji mapato.

Ifike mahala mbadilike, vipeni hivi vilabu uwezo wa kuwekeza kwenye viwanja vyao wenyewe na kuvitumia badala ya kuutegemea uwanja wa taifa. Ule ubakie kuwa uwanja wa mechi za kimataifa na michezo mingine na paheshimike na kila mwananchi.
 
...
...
...
Leo Azam wananyimwa haki kutumia uwanja wao wa nyumbani kwa mechi zake za nyumbani sababu tu TFF wanajua watakosa pesa kuneemesha matumbo yao, hii inakatisha tamaa vilabu vyetu kuongeza wigo wa mapato yake kwa mechi ambazo zingechezewa kwenye viwanja vyao.
...
...
...
Hili la msingi sana, ule Uwanja wa Azam ni mzuri kuliko viwanja vingi tu nchini, TFF waache urasimu wawaruhusu Azam watumie Uwanja wao.
 
Yaani mpira wa bongo ni zengwe tu kuanzia shirikisho mpaka timu hizo zinazoitwa kongwe yaani wanadeka kama watoto
 
Back
Top Bottom